Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za asili nchini Saida Karoli,
amezikanusha tetesi zilizoanza kuenea tangu jana kuwa amefariki kwenye
ajali ya boti katika ziwa Victoria.
Akiongea kwa simu leo asubuhi , Saida ambaye baada ya
kutumbuiza kwenye tuzo za Kili wiki iliyopita alielekea Makongorosi
Chunya mkoani Mbeya, amesema yupo hai na ni mzima wa afya.
“Mungu wangu, mimi niko hai, ndugu yangu, naomba uwaeleze watanzania
kwamba Saida ni mzima, hakuna chochote kilichotokea hata mimi mwenyewe
nimeshangaa yaani watu wanapiga simu, ni suala la msiba lakini si
kweli,” amesema Saida.
0 comments:
Post a Comment