Sunday, 4 August 2013

LEO KATIKA HISTORIA: HEKALU LA PILI MJINI JERUSALEM LILIVUNJWA NAMAJESHI YA KIRUMI




Agosti 3, 70 A.D
Warumi walilivunja hekalu la pili la Suleiman mjini Yerusalem.
Hii ilikuwa ni vita ya kuamua mwisho wa Vita ya kwanza kati ya Wayahudi na Warumi. Mapambano ya kuitaka Israeli hususani mji wa Jerusalem yalianz amuda mrefu lakini mwaka 66 AD warumi waliuteka mji huo.
Chini ya Uongozi wa Emperor Titus akiasidiana na Tiberius Julius Alexander katika Jeshi la Warumi  waliuteka mji wa Yerusalem.
Wayahudi walishindwa kupigana katika vita hii kutokana na kukosa umoja, uongozi uliosimama, malumbano ya wao kwa wao hali iliyowafanya wakose mazoezi na maamdalizi ya vita iliyokuwa ikiwakabili.
Hekalu la Pili ndilo lililokuwa maarufu, limekuwa na kumbukumbu hata ukifika hii leo katika Jiji la Rome utakutana na Mnara wa Titus wakisherehekea kuiteka Yerusalem na Hekalu.  
Uyahudi hadi leo wanalia na kuomboleza kutekwa  na kuvunjwa kwa hekalu katika sherehe zinazojulikana kwa jina la Tisha B’Av.
 

0 comments:

Post a Comment