Agustina Dorman katika picha tofauti, na kulia akiwa na mwanae wa miaka mitatu. |
Mwanamke mmoja ambaye alianza
kuchipuka nywele nyeusi usoni kwa miaka 19 baada ya kujifungua mtoto
wake wa kwanza anasema hataki tena kuficha ndevu zake.
Raia wa Indonesia Agustina Dorman, mwenye miaka 38, kwanza aligundua kukua kwa ndevu fupi wakati alipokuwa na miaka 25, siku kadhaa baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza.
Tangu wakati huo alikuwa akijificha uso wake kwa kujifunika hijabu kila napotoka nje kwenye kijiji cha Penaga, nchini Indonesia.
Lakini ni yeye aliyeamua kutupa mavazi hayo na kukubali hali yake - bila kujali kukodolewa macho na kushangaa kusikokuwa kwa lazima ambavyo sasa anashawishi.
Agustina - ambaye pia ana sharubu na nywele za kifuani - anasema kwamba kila anapokusudia kukata au kunyoa ndevu hizo anakabiliwa na maumivu yasiyovumilika.
Baada ya majaribio kadhaa kujiepusha na ubeberu huo, alilazimika kuziachia ziendelee kukua.
Na alihofia kwamba watoto wake - wenye umri wa miaka 19 na mitatu - wangenyanyaswa kutokana na muonekano wa mama yao, Agustina alijificha kwenye hijabu.
Miongoni mwa idadi kubwa ya Waislamu nchini Indonesia, Agustina aliweza kujipenyeza bila kushawishi mshangao usio wa lazima.
Lakini anasema mtoto wake mkubwa alianza kupokea dhihaka kutoka kwa wengine ambao waligundua kuhusu hali ya mama yao isiyokuwa ya kawaida.
Ilimfanya binafsi kuwakabili wanaowasumbua watoto wake kwa kujifunia mwenyewe na kutembea huru kuzunguka kijiji chao kwa mara ya kwanza wiki hii.
Anatumaini kwamba kupitia elimu kuhusu hali yake, watu watakuja kukubaliana na muonekano wake.
Mapema mwaka huu msichana mwenye ndevu wa Ujerumani aitwaye Mariam alijitokeza kwenye kipindi cha Uingereza 'This Morning' kufichua kwamba anajihisi mwenye mvuto kwa ndevu zake fupi ngumu.
Mariam sasa husafiri na kama msichana mwenye ndevu za kuigiza, ambapo anasema anafurahia tangu alipojifunza kuigiza siku zilizopita na pia hupenda kuelimisha watu kuhusu suala hilo.
Alisema: "Nataka kuwapa watu fursa ya kuongea na msichana mwenye ndevu, sababu kwa kawaida wanahofia mno katika mitaa".
0 comments:
Post a Comment