Tatizo la ukahaba linaonekana kukua nchini, likiwemo Jiji la Dar es Salaam, kwa watu kufanya vitendo hivyo kwa staili tofauti.
Huku baadhi ya watu wakidaiwa kufanya
ukahaba ofisini kwa kuvaa mavazi yasiyo na staha, kwa lengo la kuwawinda
wanaume, baadhi yao wanajiuza waziwazi mitaani hasa nyakati za usiku,
achilia mbali wale wanaojiuza mchana kwa kusimamisha watu na kujifanya
wanaomba msaada au lifti za magari kisha anaomba namba ya simu.
Ahadi nyingi zimetolewa na Serikali
kuhusiana na kukomesha biashara hii chafu, bila mafanikio, huku swali
kuu likiwa ni nani hasa wananunua makahaba?
Utafiti unaonyesha kuwa wanunuzi wakuu
wa makahaba ni watu wenye hali ya wastani kimaisha, wakiwemo waume za
watu, huku baadhi ya wale wanaojiuza ni wake za watu. Sababu kubwa ni
migogoro katika ndoa, tabia tu za mtu mwenyewe kupenda ngono na matatizo
mengine ya kiafya na kiuchumi.
Biashara haramu hadharani
Ni jambo la kushangaza, lakini ndicho
kinachozungumzwa kwamba kuna madanguro yameanzishwa katika baadhi ya
mitaa ya jiji la Dar es Salaam, watu wazima pia wakiwemo watoto
wanajiuza.
Madanguro hayo yaliyopo eneo la
Buguruni Madenge imedaiwa kuwa ni chanzo cha watoto hasa wa kike kuacha
shule na kujiingiza kwenye ukahaba.
Jumla ya madanguro 15 yenye vyumba 170
yapo eneo hilo la Buguruni Madenge, huku yakitishia kuharibu mwelekeo wa
watoto wanaoishi jirani na madanguro hayo hasa baada ya kuonekana
baadhi yao kujiingiza kwenye ukahaba. Wakazi wa eneo hilo sasa wameonya
kwamba watachukua hatua za kuyafunga madanguro hayo, baada ya kile
wanachosema kwamba Serikali ni kama haitaki kufanya hivyo.
Wametangaza kuwa kabla ya mwisho wa
mwezi huu, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala ayafunge
madanguro hayo, asipofanya hivyo wataandamana kuelekea kwenye ofisi ya
Kamanda huyo, huku wengine wakisisitiza kwamba watayafunga kwa nguvu.
Wananchi waandamana
Hivi karibuni baadhi ya wakazi wa eneo
hilo waliandamana hadi kwenye ofisi ya Serikali ya mtaa wao huo,
wakiushutumu uongozi wa Serikali hiyo kwa kushirikiana na baadhi ya
Polisi, kwa kile walichodai kwamba kuna mazingira kama vile wanapokea
rushwa kutoka kwa wamiliki wa madanguro hayo ili yasifungwe.
“Sitaki
kuamini kama kweli Serikali au polisi hawajui kinachoendelea kwenye
madanguro haya. Hata kama hawajui, kwanini tunapolalamika kwenye vyombo
vya habari kama hivi hakuna hatua za maana zinazochukuliwa,” anahoji Thadei Hamdani.
0 comments:
Post a Comment