Kuna faida nyingi za kula matunda licha ya kupenda ladha
tamu za matunda tunayokula. Matunda yana
virutubisho vingi ikiwa vitamin A na C hupatikana kwenye matunda mengi
ukilinganisha na virutubisho vingine vilivyopo kwenye matunda mengine.
Matunda husaidia kupunguza matatizo ya moyo( heart
diseases ), stroke ( kiharusi ), shinikizo la damu ( blood pressure ), cholesterol,
aina mbalimbali za saratani (cancer ), matatizo ya uwezo wa macho kuona na
mengine mengi.
Matunda yote yana manufaa kwa miili yetu lakini napenda
ujue haya machache kuhusu faida za apple, parachichi, ndizi, zabibu, embe, chungwa,
papai na nanasi. Matunda haya niliyoyataja huwa tumezoea kuyala lakini naamini
wengi wetu hatujui sana kuhusu ni vitu gani tunanufaika kutokana na kula matunda haya.
Zijue faida za matunda.....
APPLE.
-Hupunguza uwezekano wa kupata kisukari ( diabetes ) na
pumu (asthma )
-Husaidia kinywa kutokuwa na harufu mbaya ( natural mouth
fresher ) vilevile apple husafisha meno
kila unapotafuna.
Je Unajua? Harufu nzuri ya apple hupatikana kwenye
maganda/ngozi yake, hivyo ni vyema ukalitafuna pasipo kulimenya kwani vitamin
nyingi pia hupatikana kwenye maganda/ngozi ya juu.
PARACHICHI.
-Ni chanzo cha vitamin E.
-Hupunguza kiwango cha cholesterol mwilini.
-Kwa afya njema ya moyo wako, kwenye sandwich au mkate
tumia parachichi badala ya siagi.
Je Unajua? Watoto hupenda sana kula parachichi kwasababu
ni laini na pia mafuta ya parachichi husaidia katika kukuwa kwa mtoto na
kuwa mwenye afya bora.
NDIZI.
-Ni chanzo cha vitamin B6 na madini ya potassium.
-Licha ya kuwa na ladha nzuri, ndizi zina madini mengi ya
potassium ukilinganisha na matunda mengine ambayo husaidia kupunguza ongezeko
la shinikizo la damu ( blood pressure ).
Je Unajua? Watu wenye aleji na material ya mpira( rubber
latex ) wanaweza pia kuathirika kwa aleji ya ndizi kwakuwa mpira na ndizi vyote
zina aina moja ya protini.
ZABIBU.
-Ni chanzo cha madini ya manganese.
-Hupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya moyo kwa
kusaidia kushusha kiwango cha shinikizo la damu ( blood pressure )
-Huepusha magonjwa ya aina mbalimbali za saratani kwa
kuzuia usambaaji wa seli za saratani ya titi ( breast cancer ), tumbo ( stomach
cancer ) na utumbo ( colon cancer ).
Je Unajua? Unaweza gandisha zabibu za kijani na nyekundu
na ukazitumia kama barafu ( ice cubes ) kwenye kinywaji chako upendacho.
EMBE.
-.Ni chanzo cha vitamin A na E.
-Vitamin A iliyopo
kwenye embe husaidia kuboresha macho yako kwa kukuwezesha uweze kuona vizuri.
Pia husaidia kupunguza uwezekano wa upofu kwa wazee kwa kuimarisha macho yao.
Je Unajua? Embe ni tamu sana
likiwa limeiva lakini pia likiwa bichi unaweza kutumia embe kutengenezea
kachumbari, achali, chutney na salad
CHUNGWA.
-Ni chanzo cha vitamin C na
madini ya potassium.
-Chungwa lina vitamin
inayojulikana kama ‘’folate’’ ( B-Group Vitamin ) ambayo husaidia katika
kujengeka kwa ubongo wa mtoto kwa mama mjamzito.
-Chungwa lina kemikali
zinazojulikana kama ‘’hesperidin’’ ambazo hupunguza kiwango cha cholesterol
kwenye damu.
Je Unajua? Sehemu nyeupe ya
chungwa ( gome lililo ndani ya chungwa ) lina thamani ya vitamin karibia sawa
na nyama ya chungwa hivyo ni vyema kula chungwa lote baada ya kumenya maganda
yake.
PAPAI.
-Ni chanzo cha vitamin A na C.
-Papai lina enzyme ijulikanayo
kama ‘’papain’’ ambayo husaidia katika kusaga au mmeng’enyeko wa chakula.
-Pia vitamin A iliyopo kwanye
papai husaidia husaidia kuboresha afya ya ngozi yako.
Je Unajua? Mbegu nyeusi za
papai zinaweza kuliwa japo kuwa ni chungu lakini unaweza kuzisaga na salad kwa
kutumia blender badala ya pili.
NANASI.
-Nanasi lina enzyme asilia
ijulikanayo kama ‘’bromelain’’ ambayo husaidia kuvunjavunja protini hivyo husaidia katika mmeng’enyeko wa
chakula.
-Vilevile enzyme ya bromelain
husaidia kupunguza ukuaji wa seli za saratani na kuchochea uponaji wa vidonda
kwa haraka.
Kwa hayo machache hapo juu
unaona ni jinsi gani matunda yalivyo muhimu kwa kujenga afya zetu na kutumika kama dama kwa miili
yetu. Napendekeza upende kula angalau tunda moja kwa siku kwa uboreshaji wa
afya yako.
0 comments:
Post a Comment