|
Safari Imeiva baada ya kuvamiwa Alfajiri |
|
Makazi yao hata kwa Mtogole kuna nafuu |
|
Waliokubali kuondoka, na mifuko ya Ki Nigeria kama uswazini kwetu |
Lile kundi la watu zaidi ya 62 ambalo limekuwa kero kwa zaidi ya wiki
kadhaa katika mitaa ya Hyde park Karibu na Hotel kubwa ya Kifahari ya
Dorchester Hotel huko Uingereza. Raia hao kutoka Romania waliweza
kujenga makazi yao duni katika eneo moja la wazi kitendo ambacho
kilikuwa kinawakera wenyeji wa hapo kwani licha ya kuwa wanachafua
mazingira, wageni hao walikuwa na kawaida ya kuomba omba misaada toka
kwa wakazi na wapita njia.
Asubuhi ya Leo kundi la Askari Polisi walifika katika eneo hilo na
kuwaeleza ya kwamba kwa hiari yao waondoke kwao na ndege ipo ya bure au
wanaotaka kubaki basi wataenda jela. Katika Umati huo wote, ni watano tu
waliokuwa na kibali ya kuishi na kufanya kazi nchini humo.
Haya sasa" Nani Kasema Ulaya Hakuna Omba Omba?"
0 comments:
Post a Comment