BILA kocha hakuna ushindi hapa Afrika
Kusini, Manchester City imemaliza mzunguko wa kwanza wa ziara yake ya
kujiandaa na msimu kwa maumivu mjini Durban.
Kuondoka ghafa kwa kocha Manuel
Pellegrini na kutowasili kwa Alvaro Negredo na Stevan Jovetic kumeifanya
City ifungwe kwenye Uwanja wa Moses Mabidha kwa bao la dakika za lala
salama la penalti.
Kilikuwa kipigo cha pili baada ya
Jumapili kuchapwa mabao 2-0 na SuperSport mjini Pretoria, kocha
Pellegrini akiukosa mchezo huo baada ya kusafiri ghafla kurejea nyumbani
kwao Chilekumuuguza mama yake
La kwanza: Bongani Ndulula wa AmaZulu akifunga bao la kwanza katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester City
Kocha huyo mpya alipanga kikosi cha
kucheza mechi hiyo kabla ya kuondoka kwenda Santiago, akimuanzisha
mchezaji mpya aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 30, Fernandinho sambamba
na Yaya Toure katika safu ya kiungo kwa mara ya kwanza.
Wachezaji wa Pellegrini bado
wanachanganya taratibu baada ya kurejea mazoezini kiasi kama cha wiki
mbili kutoka mapumzikoni na David Silva na mchezaji mpya, Jesus Navas –
ambaye ataungana na Negredo na Jovetic hawajaripoti.
La kusawazisha: James Milner aliisawazishia Manchester City
Ameondoka: Manuel Pellegrini amerejea nyumbani Chile kwa matatizo binafsi
Mabao ya Amazulu yalifungwa na Ndulula dakika ya 20 na Van Heerden kwa penalti dakika ya 87, wakati la City lilifungwa na Milner dakika ya 26.
Mabao ya Amazulu yalifungwa na Ndulula dakika ya 20 na Van Heerden kwa penalti dakika ya 87, wakati la City lilifungwa na Milner dakika ya 26.
Kikosi cha Amazulu kilikuwa: Kapini; Macala, Teyise, Msekeli, Hlanti; Madondo, Madubanya, Manqana, Zondi, Dlamini; Ndulula.
Man City: Hart/Pantilimon
dk63, Richards/Zabaleta dk46, Kompany/Garcia dk46, Nastasic/Lescott
dk69, Kolarov/Boyata dk75, Milner/Razak dk75, Toure/Rodwell dk46,
Fernandinho/Barry dk69, Sinclair, Dzeko/Nimely dk75 na Nasri/Suarez
dk69.
Mashabiki: Mashabiki wa Afrika Kusini wakiisapoti Man City
Nahodha wa City, Vincent Kompany akimiliki mpira
Edin Dzeko akijaribu kupasua ukuta wa Amazulu
Samir Nasri akiambaa na mpira
0 comments:
Post a Comment