Wednesday, 17 July 2013

MSANII FRANK ATISHIWA KUUWAWA....!!

MSANII wa Filamu za Kibongo, Mohammed Mwikongi ‘Frank’ amedai kutishiwa kuuawa baada ya kupokea ujumbe mfupi wa meneno ‘sms’ kutoka kwa mtu anayekulikana kwa majina ya Jonathan Lyradu.
 
Mohammed Mwikongi ‘Frank’.
Frank amesema alianza kupokea meseji hizo tangu mwezi uliopita ambapo Lyradu amekuwa akimtishia kusitisha pumzi yake hapa duniani.
 
“Mara ya kwanza nilijua amekosea namba, nikamuuliza anamuhitaji nani, lakini akanitumia meseji nyingine na kunitaja jina langu huku akiendelea kunitisha na kunimwagia mvua ya matusi kwa kweli nilimshangaa kwani simjui mtu huyo,” alisema Frank.
 
Msanii huyo alisema ametoa taarifa katika Kituo Kidogo cha Polisi Tabata na kufungua jalada TBK/RB/2750/13 TAARIFA.
 
Katika utafiti wa awali uliofanywa na polisi wakati wa kumsaka mtu huyo anayemtishia maisha Frank anaonekana katika mitandao kuwa ni mkazi wa maeneo ya Magomeni, Sinza na Bamaga, Mwenge jijini Dar.
Credit:GLP

0 comments:

Post a Comment