Bondia Thomas Mashali akionesha midoli yake anayoifananisha na mabondia wenzake, Kalama Nyilawila (kushoto) na Mada Maugo, wakati wa mazoezi yake yanayoendelea katika gym yake iliyopo Manzese, Dar es Salaam (HM)
Akizungumza na katika gym yake, Manzese, Dar es Salaam jana, Mashali alisema mabondia hao hawana uwezo wa kupambana naye kwa sasa na ni kama midoli kwake.
Mashali, ambaye atapanda ulingoni Oktoba 30 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kuzichapa na Maugo, yuko katika mazoezi makali kwa ajili ya pambano hilo kabla ya baadaye kupigana na Nyilawila.
"Unajua hawa ni kama midoli kwangu (huku akionesha midoli aliyoshika), na kwa kudhihirisha hilo nitaanza na maugo Oktoba 30 kumuonesha kuwa hatakiwi kuzungumza asichokijua," alisema Mashali.Alisema anaamini uwezo wake wa sasa utakuwa wa juu zaidi ya Maugo na Nyilawila, ambapo alipata sare alipopigana na Nyilawila.
Katika pambano hilo la Mashali na Maugo la Oktoba 30, kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi, ambapo Ibrahim Class 'King Class Mawe' atapanda ulingoni kupambana na Halid Manje katika mchezo wa raundi sita. Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zitakazokuwa zikisabazwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' DVD hizo mpya ni kati ya mike tyson vs evander holyfield na felix trinidad vs roy jones jr Felix 'Tito' Trinidad vs Pernell Whitaker . Chanzo: shaffihdauda
0 comments:
Post a Comment