Sunday, 28 July 2013

STAREHE NA ANASA KWA WASANII CHANZO CHA KUWA WATUMWA KWA WAUZA MADAWA YA KULEVYA


Sina haja ya kutoa mifano mingi kwa sasa kwa Vile kila mtu anashuhudia wimbi la wasanii wakijiingiza katika biashara ya kuuza madawa ya kulevya, wengi wakitumika kusafirisha kutoka nchi moja kwenda nyingine ..Majuzi tumeshuudia video Model wa Bongo flava Agness na sakata lake la kukamatwa huku South Africa..na Kuna Habari kuwa kuna wasanii wengi wanaojihusisha na biashara hiyo japo bado hawajakamatwa.....
Kwa uchunguzi mdogo wa wasanii hawa hutumwa kubeba tu kutoka Tanzania na kupeleka mzigo nchi nyingine akishafikisha mzigo basi analipwa chake kidogo anarudi Tanzania Kuponda Starehe....Hii inatoka na Maisha Fake wanayoishi Wasanii wengi hapa Tanzania kwa Kutaka watu waone kuwa kazi zake za kisanii zinalipa kumbe wana njia zingine kama hizi za kujiingizia hela zisizo Halali....Wengi wa wasanii wetu hupenda kufanya starehe na anasa sehemu mbali mbali za gharama ili waonekane sasa hili linawafanya watafute hela kwa nguvu mwisho wake wanaishia kwenye madawa aka Unga ........

USHAURI....

Ni vyema wasanii wakajituma katika kazi zao na kuzifanya zilepe ili waweze kufanya maisha wanayo yaota kuliko kujiingiza katika janga hili la madawa ya kulevya...na kwa Habari nilizozipata kwa sasa watanzania wanachunguzwa sana wakiingia nchi za watu kwa kila kinachosadikika kuwa tumezidi kufanya biashara hiii..


0 comments:

Post a Comment