Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali nchini imesema karibu nusu ya watu waliojitokeza kupima vinasaba (DNA) ili kubaini uhalali wa watoto wao, vipimo vimeonesha si wazazi halisi wa watoto waliopimwa.
Takwimu
hizo ni kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2010, ikionesha
kuwa,
asilimia 48.32 ya wazazi 'wanalea' watoto wasio wa kwao wakati asilimia 51.68 ndio wazazi halali.
Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Jinai, Vinasaba na Baiolojia wa ofisi hiyo, Gloria Machuve katika mkutano na wanahabari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dar es Salaam.
Ingawa hakutaja idadi kamili ya waliojitokeza kupima DNA, alisema idadi hutofautiana mwaka hadi mwaka. Ili kufanya vipimo vya DNA, wazazi hulazimika kulipia Sh 100,000.
Machuve alisema kazi ya DNA si kutambua watoto halali na wasio halali pekee, bali vipimo hivyo vina umuhimu mkubwa kwa jamii.
Alitoa mfano kuwa, matumizi ya Teknolojia ya vinasaba vya binadamu yamewezesha kesi mbili za mauaji ya vikongwe na albino kutolewa hukumu katika mikoa ya Shinyanga, Kagera na Sumbawanga baada ya kufanyika kwa uchunguzi katika matukio manane.
Aidha, alisema katika majanga mbalimbali yaliyokumba nchi ikiwa pamoja na milipuko ya mabomu yaliyotokea Mbagala, Dar es Salaam mwaka 2010 walitambua mabaki ya askari sita ambao baadaye walichukuliwa na ndugu zao na kuzikwa.
Alitolea pia mfano wa tukio la moto katika Shule ya wasichana ya Idodi mkoani Iringa ambako licha ya kuungua vibaya, miili ya wanafunzi 12 ilitambuliwa hivyo makaburi yao kutambuliwa. Katika Jengo la ghorofa lililoporomoka mtaa wa Kisutu mwaka huu, marehemu 23 walitambulika.
Aidha, katika ajali ya Ndege ya Comoro mwaka 2010 mabaki ya miili ya marehemu 25 ilitambuliwa huku katika masuala ya uhamiaji teknolojia hiyo ilitumika kudhihirisha hawana uhusiano na wananchi wa Tanzania.
Machuve alisema katika masuala ya ubakaji na mimba za utotoni teknolojia hiyo imesaidia kuwa fikisha wahusika mahakamani pamoja na katika wizi wa kutumia silaha.

0 comments:
Post a Comment