ARUSHA:
(JAIZMELALEO)-Muuguzi wa Hospitali ya KCMC mjini Moshi aliyefahamika kwa jina
la Renalda Nemes Minja ameuawa kwa kunyongwa na waya wa umeme Jijini Arusha
imebainika.

Hata
hivyo chanzo kingine kimedai kwamba muuguzi huyo mwenye umri wa miaka 32
alikuwa na tabia ya kutoka na wapenzi wengine nje ya mpenzi wake.
Pia
ilikuwa ni tabia yake kupata mapumziko Jijini Arusha kila mwishoni mwa juma
endapo hayuko katika zamu hospitalini hapo, kiliongeza chanzo hicho.
Hadi
mauti yanamkuta alikuwa Jijini Arusha.
Jeshi
la Polisi mkoa Arusha limesema mwili wa Marehemu ulikutwa katika Hoteli ya Home
Suit iliyopo Mianzini Jijini Arusha.
Aidha
Kaimu Kamanda wa Polisi Arusha, Japhat Lusingu amesema muuaji amefahamika kwa
jina la Letare Lema (40) mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Lusingu
amekitaja chanzo cha mauaji hayo kuw ani wivu wa mapoenzi ndio ulisababisha
muuaji kufanya unyama huo.
Pia
Kaimu Kamanda huyo amesema Muuaji amekamatwa na yupo mahabusu kwa mahojiano
zaidi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru.
0 comments:
Post a Comment