Saturday, 24 August 2013

AFUNGIWA PANGONI KWA MIAKA 30 NA WAZAZI WAKE KWA KUONESHA DALILI ZA UKICHAA...

KUSHOTO: Dong Watou akionesha kovu refu pajani mwake. KULIA: Dong Hai akiwa amejikunyata (kulia) pangoni mwake.
Mwanaume ambaye alionesha dalili za matatizo ya kiakili wakati akiwa kijana mdogo alifungiwa pangoni na wazazi wake kwa miaka 30.

Dong Hai, miaka 46, aliwekwa pangoni kwenye makazi yenye ukubwa wa mita za mraba tano nyuma ya nyumba ya wazazi wake baada ya kuhofia kwamba angeweza kuwadhuru wengine.
Dong Watou na mkewe Xiao Hing kutoka Longhai, jimbo la kusini mashariki mwa China la Fujian alisema waliomba msaada kwa hospitali kadhaa pale mtoto wao pekee wa kiume alipodhoofu na kuhofia afya yake ya kiakili.
Walikwenda hospitali kadhaa jimboni humo lakini walirejea bila mafanikio. Wanandoa hao walitumia akiba yao yote kwa matibabu katika mwaka na walilazimika kusitisha matibabu ya kijana wao huyo.
Huku muda ukisonga mbele kwa wanandoa hao, ambao sasa wanakaribia umri wa miaka 70, wamesema hofu yao kubwa kabisa ni kitakachotokea kwa Hai watakapokuwa wamekufa.
Nyumba ya wanandoa haina tofauti na nyingine katika kijiji hicho, isipokuwa makazi hayo ya pangoni katika kiwanja chao.
Hai hakuwahi kutoka nje ya kibanda hicho kwa miaka 30 iliyopita.
Chakula hupenyezwa kwake kupitia kwenye tundu ukutani na kila siku baba wa Hai hutumia upawa, ambao umefungwa katika ncha ya nguzo ndefu ya mwanzi, kuondoa kinyesi.
Mama wa Hai kisha hunyunyiza maji ndani kusafisha sakafu na mtoto wake huyo.
Miaka kadhaa iliyopita, ardhi ya kijiji hicho ilitaifishwa na serikali kwa ajili ya kuendelezwa, na wanandoa hao wazee wakapoteza chanzo chao cha mapato.
Sasa wanafanya kazi za vibarua kuweza kuendesha maisha yao.
Mwaka jana Dong Watou aliyekuwa akifanya kazi kama mlinzi kwenye eneo la ujenzi kijijini hapo, na alipigwa na dereva aliyekuwa amelewa pombe. Sasa mguu wake wa kulia bado una kovu refu na hawezi kufanya kazi zozote ngumu.

0 comments:

Post a Comment