Watumishi wawili katika zahanati ya Mwanhala wilayani Nzega, wamekumbwa na kashfa ya kufanya mapenzi na wagonjwa hospitalini. |
Kutokana
na kashfa hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Bitun Msangi, ameiagiza
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa
watumishi hao.
Agizo
la mkuu huyo limetolewa hivi karibuni, baada ya Diwani wa kata ya
Utwigu, Sawaka Shita kuwalalamikia watumishi hao mbele ya Baraza la
Madiwani, kwa kukithiri kufanya mapenzi na wagonjwa nyakati za kazi,
licha ya kuonywa kwa mara kadhaa.
Diwani huyo aliliambia baraza hilo kuwa vitendo hivyo vina
hatarisha maisha ya watumishi hao na ya wananchi, hususani waliotembea nao na kutishia kuvunja ndoa za wananchi.
Alidai kuwa taarifa hizo za malalamiko, zilishafika katika
ofisi
ya Mkurugenzi Mtendaji, tayari kwa utekelezaji, lakini wananchi wa
kata hiyo walitaka kuifunga zahanati hiyo, baada ya kukithiri vitendo
hivyo vya kufanya mapenzi katika wodi zilizopo.
Aliomba
baraza liwahamishe na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu watumishi
hao, ambapo majina yao yamehifadhiwa kwa usalama wao, huku jitihada za
kuwachukulia hatua zikifanyika.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Patric Mbozu alisema
suala hilo ni la hatari na linapaswa kufuatiliwa kwa umakini ili
lipatiwe ufumbuzi na wananchi waendelee kupatiwa huduma za tiba.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri hiyo, Abraham Mdeme alikiri kupokea malalamiko
hayo na kuahidi kuwa suala hilo, litafuatiliwa mapema ikiwemo
kuwahamisha kwa kufuata taratibu zilizopo.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Msangi alisema watumishi hao,
wamevunja maadili ya afya, hususani kufanya ngono katika wodi za zahanati kwa nyakati za kazi.
0 comments:
Post a Comment