Wakati
bado kuna maswali mengi kuhusu magaidi waliohusika na shambulio la
Westgate kama kweli waliuawa kama isemavyo taarifa ya serikali ya Kenya,
mtandao wa Mirror umetoa taarifa kuhusu tetesi za uwezekano wa magaidi
hao kutorokea njia ya maji taka kutoka katika jengo hilo.
Mtandao huo umedai kuwa baadhi ya magaidi walitoroka kupitia njia ya
maji taka iliyoko chini ya jengo la Westgate inayoenda kutokea katika
mto Nairobi.
Kwa mujibu wa habari hiyo njia hiyo inaanzia eneo la maegesho ya magari
katika jengo la Westgate na inaenda moja kwa moja kutokea katikati ya
jiji la Nairobi. Magaidi hao wanahofiwa kutumia njia hiyo ya maji taka
kutoroka na kuwaacha wengine wakiendelea kushambulia.
Taarifa hiyo inaendelea kudai kuwa wana usalama wanadai kuwa magaidi wa
Al-shabaab walisafiri umbali wa nusu maili kwa magoti katika njia hiyo
ya chini ya ardhi katika njia ya maji taka.
Chanzo kimoja kilisema “They escaped like sewer rats. The terrorists
would have been able to pass through the underground tunnels at a rapid
pace and surface almost unnoticed”.
Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa wachunguzi wa Kenya hawakuigundua
njia hiyo ya kutorokea mpaka masaa 72 kupita baada ya shambulio kutokea.
Hapa ndipo inapotokea njia hiyo ya maji taka kutoka Westgate hadi katikati ya jiji la Nairobi
0 comments:
Post a Comment