Wapendwa wasomaji wa safu hii, huu ni muendelezo ya makala yetu ya wiki iliyopita inayozungumzia mambo ambayo mwanamke hapaswi kuyafanya awapo faragha na mwenza wake.
Hiyo ni tabia mbaya, ni ubinafsi. Kama kweli unampenda mwenzi wako hutakubali kushiriki naye bila mawasiliano ya hatua kwa hatua. Kumbuka kwamba mnachokifanya siyo kitendo cha ubakaji, umeridhia kwa moyo wako mkunjufu. Unataka raha, sasa utazipataje ikiwa kila mmoja anafanya anachokijua?
Kitendo husika kinamaanisha umoja, unatakiwa uhakikishe unamteka hisia zake zilalie kwako, nawe pia zako uzilaze kwake. Msome ujue anachokitaka kisha mtendee yale yanayompendeza. Ukiona naye anapoteza mawasialiano na wewe, muweke sawa.
Katika hili, nifafanue kwamba kuna wakati mwanamke anakubali kwenda faragha na mwanaume ambaye kwa hakika hampendi. Katika kipengele hicho, matokeo hayawezi kuwa mazuri. Mvuto wake kwako hauwezi kuwa barabara kama hakuna nguvu ya asili inayowavuta na kuwaweka pamoja.
Hiyo nguvu ya asili ni upendo, yaani wewe na yeye mnapendana, kwa hiyo hata tendo lenyewe linakuwa linaleta raha. Kama humpendi maana yake utakuwa unajilazimisha. Hakuna nguvu ya asili inayoweza kukuvuta kwa ndani ili ufurahie kile ambacho mtakuwa mnakifanya.
Ipo tabia kwa baadhi ya wanawake ya kudhibiti hisia zao ili zisiendane na za mwenzake. Unakuta ni ukweli kwamba anapokea mcharazo unaofaa, naye anausikilizia lakini mwenyewe anajitahidi kujikausha eti asijioneshe kwa imani kwamba anapoonekana mahututi, mwenzi wake atamtesa.
“Aku, mimi sitaki kabisa mwanaume aone udhaifu wangu kwake tunapokuwa kitandani, akijua ananipatia atavimba kichwa halafu atanitesa kwa kiburi chake,” hiyo ni kauli ambayo ilitoka kwa mwanamke mmoja ambaye nilipata kubadilishana naye mawazo, wakati nikifanya utafiti wa mada hii.
Yupo msomaji wangu mwanaume aliwahi kuniambia: “Nina tatizo kubwa sana na mke wangu, hataki kuonesha hisia zake, anajikausha hata sijui nifanye nini. Hapa nilipo sijui kinachomfanya asisimke wala sijui ni wakati gani na lini amewahi kufika kileleni. Hili ni tatizo linalonisumbua.
“Nimejaribu kuzungumza na mke wangu mara kadhaa lakini amegoma katakata kuniambia kitu kinachomfanya afurahie tendo. Hataki kunishirikisha kwa chochote, anasema akiniambia ukweli nitampatia na baada ya hapo nitamnyanyasa kwa sababu hatakuwa na ujanja kwangu.”
Nikamuuliza msomaji wangu: “Ni kweli ukijua utamnyanyasa?” Akajibu: “Hata kidogo, siwezi kuthubutu. Lengo langu ni kujua jinsi ya kumfurahisha yeye. Ni mwanamke wangu, sasa atapewa raha na nani ikiwa mimi simpi? Imani yake mbaya inanikosesha raha, maana sizijui hisia za mke wangu.”
Katika mapenzi, ushamba ukae pembeni. Unapoamua kuingia faragha ni sharti ufuate mambo yote muhumu yapasayo eneo hilo. Tambua upo na mwenzio, naye ajue yupo na wewe. Baada ya hapo sasa ni kazi moja tu, kutenda kilicho sahihi bora kwa ushirikiano wa hali ya juu. Hakuna kutegeana.
Itaendelea wiki ijayo.
GPL
0 comments:
Post a Comment