Sunday, 21 July 2013

JACKLINE WOLPER AKIRI AFYA YAKE INACHUNGULIA MAUTI MUDA WOWOTE

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameeleza kuwa, tatizo alilonalo la presha ya kushuka huenda siku moja likawa chanzo cha kifo chake kwani linapomjia, huwa katika hali mbaya sana.
Akizungumza hivi karibuni Wolper alisema, tatizo hilo amekuwa nalo kwa muda mrefu na kufikia hatua ya kwenda kutibiwa nchini Afrika Kusini likapungua lakini sasa limerejea na linamkosesha amani.
“Kwa kweli hili tatizo la presha ya kushuka nililonalo ipo siku litaniondoa duniani, unajua wakati mwingine hali hiyo ikinijia natokwa na damu nyingi puani, huoni ni tatizo kubwa hili!” alisema Wolper.

MTANZANIA MWENYE UTAJIRI WA AJABU ALIPOALIKWA KUTEMBELEA CHELSEA FC YA UK!!

Making a point! The Super Mogul Davis Mosha at the Chelsea Football Team's Press Conference in London.
Ed akiongea na Waandishi wa habari za Michezo wa Uingereza kwenye makao makuu ya Club ya Chelsea, anakofuatana na baba yake Super Mogul Davis Mosha kwenye mualiko maalum wa timu hiyo.
Mkurugenzi na Mmiliki wa Delina Group Inc. ya Tanzania Super Mogul Davis Mosha, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wa michezo huko kwenye Makao Makuu ya timu maarufu sana ya Uingereza ya Chelsea Football Club, ambako yupo huko kwa mualiko maalum wa timu hiyo kabambe iliyowahi kushika ubingwa wa Uingereza mara nyingi. Mkurugenzi huyo wa Kampuni kubwa ya Delina Group Inc. inayohusika na usafirishaji wa mafuta katika Afrika Mashariki na ya kati, na ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa timu maarufu ya Yanga Afrika ya hapa nchini, anafuatana pia na mtoto wake wa kiume Ed kwenye safari hiyo. 
- See more at: http://williammalecela.blogspot.com/2013/07/mtanzania-mwenye-utajiri-wa-ajabu.html#sthash.5PCyIyKv.dpuf

0 comments:

Post a Comment