Timu ya Taifa, Taifa Stars inatarajia kukipiga leo dhidi ya Uganda the Crane huko Uganda.
MOJA ya
mikakati ya Taifa Stars kwenye mechi ya leo dhidi ya Uganda kuwania
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa Wachezaji wa
Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini ni kushambulia
kwa muda mwingi wa mchezo.
Kocha Kim Poulsen amesema maandalizi
ya Taifa Stars jijini Mwanza kwa ajili ya mechi hiyo ambayo Uganda
inaongoza kwa bao 1-0 yalikuwa mazuri, lakini mabao ni muhimu hivyo
watashambulia bila kusahau kulinda lango lao.
“Unapocheza mechi za aina hii za
nyumbani na ugenini, huku mwenyeji akiwa anaongoza mabao yana maana
kubwa katika mechi. Mabao yanabadili mchezo na pia wachezaji kifikra,”
amesema Kim akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Mt. Zion
ambayo Stars imefikia. (HM)
Amesema katika mechi ya kwanza
walitengeneza nafasi nyingi lakini hawakuzitumia, hivyo wamekuwa
wakifanya mazoezi ya kushambulia, jinsi ya kutengeneza nafasi, na jinsi
ya kumalizia.
“Hivyo tuko hapa (Kampala) kwa ajili
ya kufunga, ni lazima tufunge ili tuweze kuendelea na mashindano. Lakini
ngome yetu nayo ni lazima iwe makini ili kutoruhusu bao,” amesema Kim
na kuongeza kuwa kikosi chake cha kwanza ni lazima kitakuwa mabadiliko
kutoka na Mwinyi Kazimoto kuingia mitini na Shomari Kapombe kwenda
kwenye majaribio Uholanzi.
Amesema angalau kutakuwa na mabadiliko
kwa kuingiza sura mbili mpya katika kikosi cha kwanza, na kuongeza kuwa
wachezaji wanafahamu umuhimu wa mechi hiyo kwani timu ikienda kwenye
Fainali za CHAN itakuwa manufaa kwao binafsi.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi ya mwisho leo jioni Uwanja wa
Mandela ulioko Namboole ambao utatumika kwa ajili ya mechi hiyo kesho.
Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni
kwa saa za Afrika Mashariki na itachezeshwa na waamuzi kutoka
Madagascar wakiongozwa na Kanoso Abdoul Ohabee wakati mwamuzi msaidizi
namba moja ni Andirvoavonjy Pierre Jean Eric. Mwamuzi msaidizi namba
mbili ni Jinoro Velomanana Ferdinand huku Andriamiharisoa Hubert Marie
Bruno akiwa mwamuzi wa mezani (fourth official). Kamishna wa mechi hiyo
namba 38 ni Ismail Kamal kutoka Ethiopia.
Stars inatarajiwa kupangwa hivi; Juma
Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende, Aggrey Morris, Kelvin Yondani,
Athuman Idd, Salum Abubakar, Frank Domayo, John Bocco, Amri Kiemba na
Mrisho
0 comments:
Post a Comment