Friday, 12 July 2013

Marekani na Israel zapinga maombi ya Iran na Syria kupatiwa kiti ndani ya Baraza la Haki za Binaadam la UN

Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Marekani na Israel zimepinga ombi la Iran na Syria kupatiwa viti ndani ya Baraza la haki za binaadam ndani ya Umoja wa Mataifa.
Balozi wa umoja wa Mataifa ndani ya Umoja wa Mataifa, Rosemary DiCarlo amesema Kampeni za Syria na Israel hazikubaliki kwa kuwa nchi hizo zina rekodi mbaya juu ya maswala ya haki za Binaadam.
Iran na Syria ni miongoni mwa nchi saba wanaowania viti hivyo wakichuana na China, Jordan, Maldives, Saudi Arabia na Vietnam.
Kura za kuwania kiti hicho zitapigwa katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York mwezi Novemba.
Iran ni Mwanachama wa Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia maswala ya Haki za Wanawake na Syria ni mwanachama wa Kamati ya Haki za Binaadam ya Shirika la Umoja wa Mataifa, la elimu, Sayansi na Utamaduni.


Syria ilijaribu kuomba nafasi ya kiti ndani ya Baraza la Haki za binaadam mwaka 2011 lakini maombi hayo yalitupwa kando kwa sababu ya Mzozo wa Syria, na hatua ya mashambulizi dhidi ya Raia alizozichukua Rais wa Syria Bashar Al Assad katika kusitisha Maandamano yaliyokuwa yameanza.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa Takriban Watu 100,000 wameuawa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
Rekodi juu ya maswala ya Haki za Binaadam zimekuwa zikikosolewa na Waangalizi wa Haki za Binaadam kwa kile walichoeleza kuwa imekuwa ikimsaidia Assad na harakati zake za kupambana na Waasi.

0 comments:

Post a Comment