Friday, 26 July 2013

Mbunge wa Sweden aweka kimakosa picha inayoonesha sehemu zake za siri Instagram hii ni wakati akitaka kuionyesha tatoo ya Liverpool


Mwanasiasa mmoja wa Sweden anayeonekana kuwa member mzuri wa mtandao unaozidi kupata umaarufu bongo wa Instagram, katika hali ya ushabiki na kutaka kushare picha ya tattoo yake ya Liverpool FC iliyochorwa katika mguu wake wa kushoto , kwa bahati mbaya alijikuta akionesha mpaka sehemu za ‘ikulu ya mwili’.
Lars Ohly mwenye miaka 56, anayeonekana kuwa shabiki mkubwa wa timu ya Liverpool, baada ya kuweka picha hiyo bila kujua huwa ‘Mr Ohly’ pia ameonekana, aliifuta haraka japokuwa tayari watu walikuwa wameipata.

Katika hali ya utani Waziri wa mambo ya nje wa Sweeden kutoka kwa chama pinzani Carl Bildt, alimwambia bwana Ohly “Congratulations – finally, after all these years you have made a genuine public breakthrough.”

SOURCE: DAILY MAIL

0 comments:

Post a Comment