Baadhi ya waombolezaji waliofika msibani nyumbani kwa Profesa Jay, Mbezi Mwisho jijini Dar leo.
Mhariri
wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul (kushoto) akiwa na Mhariri
Msaidizi wa Magazeti ya Risasi na Amani, Erick Evarist msibani hapo.
Baba Mzazi wa Prof Jay, Mzee Haule (kushoto) akibadilishana mawazo na mzee mwenzake msibani hapo.
Nature (kushoto) na Dolo wakiwa msibani.
Prof Jay akihojiwa na Mtangazaji wa Star TV, Sauda Mwilima. Katikati ni Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Luquman Maloto.
Waombolezaji wakipata menyu.
Watu mbalimbali wamezidi kumiminika nyumbani kwa msanii wa muziki wa
kizazi kipya Bongo, Joseph Haule ‘Prof. Jay’ eneo la Mbezi Mwisho jijini
Dar kutoa pole kufuatia kifo cha mama yake mzazi Rosemary Majanjala.
Marehemu Rosemary aligongwa na gari aina ya Stallet juzi saa mbili usiku
ambapo alifariki baada ya kufikishwa katika hospitali ya Tumbi iliyopo
Kibaha, mkoani Pwani.
0 comments:
Post a Comment