Balozi wa china nchini Bw Lu Youqing akijiweka sawa kutokana eneo hilo la jiwe kuwa na upepo mkali
Viongozi wa CCM mkoa wa Iringa na viongozi wa Serikali wakiwa juu ya jiwe pamoja na balozi wa china nchini Bw Lu Youqing mara baada ya kutembelea eneo la chuo cha Ihemi Iringa leo
katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa Rhoda George akishuka katika jiwe hilo eneo la Ihemi leo
katibu wa CCM Kilolo akitafuta mawasiliano akiwa juu ya jiwe Ihemi leo
Viongozi wa CCM mkoa wa Iringa na viongozi wa serikali wakipungia mikono ndege ya balozi wsa china na viongozi wa CCM mara baada ya kutembelea eneo la Ihemi na kufurahishwa na eneo hilo |
Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salima Abri Asas kulia akiwa na katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye na mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita leo katika uwanja wa ndege Nduli |
Katika kuonyesha mikakati ya
awali ya kuanza kukifufua chuo
hicho balozi wa
chini nchini Tanzania Bw Lu Youqing leo
amekitembelea chuo hicho
chenye eneo la ukubwa wa
hekari 1900 na kuonyesha kuvutiwa
zaidi na eneo hilo.
Akielezea
mkakati huo katibu wa itikadi na
uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye
alisema kuwa CCM inaompango wa
kukiendeleza chuo hicho kwa
kushirikiano na serikali ya China .
“Leo tumekuja na
balozi wa China kwa
ajili ya kupaendeleza zaidi ikiwa
ni pamoja na kutoa elimu ya
uongozi pamoja na masuala ya ujasiriamali ambayo yatawafanya zaidi
vijana kuweza kujiajiri
zaidi”
Alisema kuwa mpango
wa kukifufua chuo
hicho unataraji kuanza mara moja
na kuwa hayo ni maamuzi ya
mkutano mkuu wa Taifa
ambayo utekelezaji wake
unaanza mara moja .
Nnauye alisema kuwa
kutokana na maamuzi hayo ya
mkutano mkuu wao
wameanza kufanyia kazi suala
hilo kwa kuwatafuta wahisani hao
kutoka China ambao
watasaidia kufanikisha ujenzi huo ambao kukamilika
kwake ni ukombozi mkubwa kwa vijana nchini nan chi nyingine .
Pia alisema kuwa
kuyumba kwa chuo
hicho kunatokana na mfumo
wa vyama vingi na kuwa kabla
ya mfumo
wa vyama vingi kuanza
chuo hicho cha
Ihemi kilikuwa kikifanya
kazi vema japo
alisema kwa sasa mkakati ni kukifufua
na kuwa chuo hicho kitakamilika
ndani ya mwaka huu .
Kuhusu aina ya mafunzo yatakayotolewa alisema kwa
sasa ni mapema sana ila mara
baada ya ujenzi kukamilika
basi aina ya mafunzo yatakayotolewa yatajulikana .
Nnauye alipoulizwa
kuhusu gharama ya jumla
itakayotumika kujenga chuo
hicho alisema kuwa kwa
sasa bado ni mapema kujua ni
kiasi gani kitatumika katika ujenzi na
kuwa hatua iliyopo sasa ni ya awali
zaidi .
Katika ziara hiyo ya
balozi wa China nchini
aliongozana na msaidizi wake Bi.Wang
Fang pamoja na katibu mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana ,katibu
mkuu wa UVCCM Taifa Martine Shegela pamoja na
viongozi mbali mbali wa
chama na
serikali wilaya na mkoa wa Iringa .
0 comments:
Post a Comment