Wednesday, 24 July 2013

Vurugu zakithiri nchini Misri


025 ced33WATU waliokuwa wamejihami nchini Misri wamewaua kwa kuwapiga risasi wafuasi wawili wa rais aliyeondolewa mamlakani Mohamed Morsi.
Wawili hao walikuwa njiani kuungana na wafuasi wengine wa Morsi waliopiga kambi nje ya msikiti mmoja mjini Cairo.
Chama cha Muslim Brotherhood, kinachomuunga mkono Mosri, kimelaumu maafisa wa usalama kwa utovu wa usalama , lakini mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema madai haya ni vigumu kuyathibitisha. (HM)
Kaskazini mwa Cairo, katika mtaa wa Mansoura,bomu lililipuka nje ya ofisi za polisi na kuwajeruhi maafisa kadhaa wa polisi pamoja na raia.
Kuna ripoti kuwa mtu mmoja alifariki. Chanzo: bbcswahili

0 comments:

Post a Comment