Fumanizi hilo lilibuliwa ambapo Judith Lekule na mume wa mwanamke
aliyetambuliwa kwa jina moja la Pendo walinaswa chumbani wakiivunja amri
ya sita ya muumba.
Kwa mujibu wa vyanzo, Judith yu mbioni kwenda kortini kwa lengo la
kumfungulia mashitaka Pendo akidai alimdhalilisha kwa kudai alimfumania
akiwa na mumewe.
“Kuna watu wanamshawishi Judith eti asikae kimya, aende mahakamani
akamshitaki Pendo kwamba alimdhalilisha kusema alimfumania na mumewe,”
kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, vyanzo vimeeleza kwamba, Judith anashindwa kuutumia ushauri
huo kutokana na ukweli kwamba, kesi hiyo inaweza kumgeukia mwenyewe kwa
sababu yeye ndiye aliyefumaniwa.
Sambamba na madai hayo, inasemekana pia kwamba mtaani anapoishi Judith
kumekuwa kuchungu kwake baada ya baadhi ya watu kutumia habari ya kwenye
gazeti kumkejeli na kumuonya akome kuwadandia waume za watu kwani si
tabia nzuri.
“Hali hiyo ya kunyooshewa vidole na watu inamnyima raha Judith,
anashindwa kutembea kwa uhuru mitaani,” alisema mnyetishaji wetu.
Nao baadhi ya marafiki wa kike wa Judhith wamehuzunishwa na kitendo cha mwenzao kufumaniwa na kupewa kipigo.
Chanzo kikaenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, ndugu wamemtaka Judith
aondoke anapoishi kufuatia kitendo alichokifanya ikielezwa ameitia aibu
familia.
Kwa upande wake, Pendo ameeleza kwamba mumewe alimuomba msamaha na
amemsamehe, yameisha pia akasema baada ya lile fumanizi, Judith
amemfuata nyumbani kwake mara mbili kwa lengo la kuomba msamaha.
“Nimemsamehe Judith lakini bado ana wasiwasi kwani amekuwa akija kwangu na hofu kwamba nitamshitaki katika vyombo vya sheria.
“Cha ajabu sasa amegeuka na kutoa vitisho, Judith ni rafiki yangu,
anajua alichokifanya ndiyo maana hata wapambe wake wanamshawishi
akanishitaki lakini moyo wake unakuwa mgumu,” alisema Pendo.
0 comments:
Post a Comment