Kwa
Wale ambao tunapata bahati ya maskio yetu kupata udaku wa hapa na pale
bila shaka tumeshawahi kulisikia hili, " Ukipiga Sipu ya Pweza Kabla ya
Mechi" Basi Uwanjani Patachimbika. Leo tutajaribu kudadavua kwa upande
wetu hili limekaa vipi?
Kwanza kabala sijaenda mbali zaidi napenda niseme
kwamba hii ni dhana ya kisaikolojia, ambayo hukupa fikra ya kimchezo
zaidi unapokuwa na mkeo, pia hukupa ujasiri na ushujaa wa kuutawala
Mchezo, ni nzuri kiupande mmoja, lakini haina 100% ukweli. Performance
yako inatokana na kujiandaa na kuwa kimchezo zaidi.
Kama nilipoeleza hapo awali kuhusu vyakula kwa ajili ya afya ya mapenzi,
nilizungumzia "nyama" (Red meat) ikichomwa huongeza mafuta na protein
ambayo uhitajika zaidi kipindi cha mchezo.
Pweza kama pweza, huangukia upande huu pia, huleta mafuta na protein,
kinachochangia zaidi ni ile imani uliyo kichwani kwako, hii hufanana na
mwanaume aliekunywa vidonge vya kuongezea nguvu za kiume, mathali
"Enjoy" au Erecta 2.5, Huwa na uhakika wa kufanya vizuri mchezoni kama
mwanafunzi aliyeingia katika chumba cha mtihani akiwa na
"Chabo/Nyenzo/Kibomu" obvious atakuwa na asilimia kubwa ya ushindi.
Kwa mfululizo huu hata karanga mbichi na maziwa
huwa na athari za kufanana na vitu tulivyoviongelea hapo juu.
3 hours ago
0 comments:
Post a Comment