Wednesday, 14 August 2013

AMERICA NEWS: MAMA ABEBA MIMBA YA BINTI YAKE AZAA WATOTO MAPACHA




Mwanamke mzee mwenye umri wa miaka 53 amejifungua watoto mapacha wa binti yake, baada ya madaktari kuthibitisha kuwa bintiye hatoweza kubeba mimba.
 
UKISTAAJABU YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI…
Suzie Kozisek (53) mama mkazi wa Iowa nchini Marekani mwenye watoto wanne amejifungua watoto wa bintiye aliyekuwa na matatizo ya via vya uzazi na Shinikizo la Damu.
Duru za Habari kutoka jimboni humo maarufu kwa jina la American Heartland zinasema mwanamke huyo mzee alitumika kwa kitaalamu “carrier” wa kubeba mayai ya binti yake kupitia njia ya “Vitro Fertilization”.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Good Morning America imesema mwezi Juni, 2011  binti yake anayefahamika kwa jina la Ashley Larkin alijifungua mtoto aliyempa jina la Harper.
Baada ya kujifungua ikagundulika Larkin ana matatizo ya via vya uzazi licha ya mayai ya uzazi “ovaries” kuwa mazima pia matatizo ya “Pulmonary Hypertension” ambayo ingemzuia kuzaa tena.
Hivyo walitokea wengi waliojitolea kuchukua mimba mingine ya binti huyo kutokana na ukweli kwamba asingeweza kuzaa kwa njia za kawaida na hata kama angebeba ujauzito angeweza kupoteza uhai wake.
Kozisek wenye watoto wane walio na umri kati ya miaka 20 na 30 alipandikizwa mbegu za kiume zilizokuwa tayari kwenye mayai ya Larkin na kisha kuwekwa kwenye Uterus yake mwezi 2012.
Shirika la Habari la ABC News linasema kazi ya kuyapandikiza mayai na manii ilifanyika Okotoba mwaka 2010 katika Kiliniki moja iliyofahamika kwa jina la Mayo nchini humo.
Mwanamke huyo mzee alipandikizwa mimba amejifungua mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.
Kozisek ambaye ni Katibu Muhtasi wa taasisi moja mjini Iowa alikaririwa akisema  kwa kipindi chote hadi anajifungua alikuwa mwenye afya tele ambaye hakuweza kupatwa na lolote baya.
Kwa upande wake Binti yake alisema watoto wake waliopewa majina ya Hallee na Hadlee anaona ni Baraka pia ni muujiza.
Daktari mmoja wa Kliniki ya Mayo aliyejitambulisha  kwa jina la Jan Jensen ambaye ndiye aliyefanya kazi ya uchavushaji huo na mtaalamu wa masuala ya Ujauzito kwa kina mama amesema Larkin alipobeba mara ya kwanza hakuwa na tatizo lolote na kwamba alikuwa mwenye afya njema kabisa.
Dk. Jensen aliongeza kusema Kozisek umri wake haviendani na kuchukua ujauzito huo hata kama ni kwa uchavushaji.
Daktari huyo ameongeza kusema anamsifu Kozisek kwa ujasiri wa kumpenda bintiye na watoto akiamini ni jambo la kushangaza lakini ndio lilivyo limetokea.
CHANZO: ABC News/Good Morning America/YAHOO News.

0 comments:

Post a Comment