Friday, 23 August 2013

HIZI NDIZO SABABU ZA KUACHIKA KWENYE MAPENZI


 
Kupenda Sana au Kumganda Mtu: Kwenye mahusiano mmojawapo anapokuwa anaelekea kumpenda mwenzake sana na kumganda husababisha mmoja wapo kumchoka mwenzake. Wote mkiwa kwenye mahusiano pendaneni sawa ili kutopelekea kuchokana.
Kukata tamaa kwenye mahusiano: Unapoonyesha namna ya kukata tamaa kwenye mahusiano au hali ya kusikiliza ya watu ni rahisi kupelekea mahusiano kuvunjiaka. Wengi kwenye mahusiano wanakaa kufikiria kuwa hadi kwenye ndoa. Hivyo unapokuwa na hali ya kukata tamaa kutokana na mazingira ni dhahiri kupelekea kuona bora mahusiano yaishe.
Kuwa mkali kwenye mahusiano: Hii ikiwa inawahusu zaidi wavulana/Wanaume wenye tabia hii kuwa kutokujali hali y ampenzi wako na kuwa mkali kwenye mahusiano. Kuto thamini kila hali ya shida au udhaifu wa mpenzi wako. Pia kuna wasichana/Wanawake ambao huwa na hali hii.
Utoto kwenye mapenzi: Hakuna masichana anayependa mvulana ambaye ana tabia za kitoto. Kama mvulana ukiwa na tabia za kitoto kama kuto kujiheshimu au kuwa mchafu kama mtoto inapelekea kupunguza mapenzi na hata kuachika.
Mavazi na Muonekano: Hakuna mtu ambaye ni mabaya, Ila unaweza kujiona ni mbaya kutokana na muonekano wako wa mavazi na unavyo ishi. Ni vyema kujiweka nadhifu kwenye mavazi ili kuto hatarisha penzi lako.
Uchafu wa Kucha na Vidole: Shughuli unazozifanya zinaweza zikawa ni zakuchafuka ila nivyema kuhakikisha baada ya hapo unaweka vidole vyako nadhifu na visafi. Kuwa makini kuzitunza kucha maana nimahususi kwenye kuamsha hisia za ngono. Hivyo unapokuwa mchafu wa kucha na vidole mpenzi wako anaweza kuku acha na kama ni wakike, mvulana kuogopa hata chakula chako.
Kuonyesha hisia: Kuwa na muonekano wa hisia za kumpenda mpenzi wako ni muhimu na unaposhindwa unahatarisha mahusiano yako hata kama unampenda.
Tamaa: Kwenye mahusiano jiepushe kuwa na tamaa ya vitu vingi. Kuwa na kiasi sio kila unachokiona au kukisikia basi uhitaji. Mpenzi wako atakuona unamchuna na kukuchoka mwishowe kukutupilia mbali.
Mizozo ya mara kwa mara: Unapokuwa na mzozo au kila mara kugomba na kumpiga mpenzi wako ni dhahiri hata kama unampenda atakuwa hana uhitaji kwako tena. Jiepusha kuwa na mzozo hata kama mwenzio amekosea mrekebishe taratibu.
Heshima kwenye mapenzi ni kitu muhimu, Haijalishi hali aliyonayo. Nidhamu ni jambo linaloweza kukufikishia malengo yenu.

0 comments:

Post a Comment