Ilikuwa tarehe 4/6/2013, nikiwa nimetoka zangu kazini nikisubiri a friend of mine ambae huwa nakuja nae town (by that time alikuwa maeneo ya Moroko) nikaamua kwenda pale church (St. Joseph for prayers). Kabla sijaingia getini, upande wa pili nikasikia mtu akiniita jina langu, akiwa kasimama pembeni ya gari. Bila kufikiria mara tatu tatu nikajua ni mtu anayenifahamu. Nikavuka upande wa pili na kumkuta uyo mtu ila kiukweli sio mtu niliyemzoea hadi kunijua jina ila yes nilishakuja nae several times to town with other people.
Akanisalimia na kuniambia kuwa several times amekuwa akija na mimi town (ni kweli mara nyingi huwa napanda taxi au private cars mida ya asubuhi kuja town) na kwa wakazi wengi wa mjini Daslam thats very common maeneo ya tabata, mbagala, mtongani, mivinje e.t.c. Akaniambia wanamsubiri rafiki yao then wanaenda where I was going (Kijichi) so tuondoke wote and I would pay TSh 2000. Nikampigia uyo rafiki yangu akaniambia kuna foleni kubwa na atachelewa. Kwa kuona kwamba its late nikaona niondoke nao as long as wanaelekea where I was going.
Niliwasikia wakimpigia uyo rafiki yao ila wakasema hapokei so tuondoke. Basi mi nilikaa back seat na gari yao ni vitz ya mlango1. Mbele walikuwa 2 na mimi nyuma. Basi safari ikaanza ila moyoni sikuhisi amani kabisa!!Nikawa natafta nione plate number za gari kwenye kioo nikagundua kuwa haikuwepo na vioo vilikuwa tinted!Kiukweli hofu iliniingia sana. Mara moja nikachukua my bible and prayer books nikapiga sala pale (im sure they saw me praying). Wakati tunaondoka walipromise kuchukua abiria wengine kituo cha stesheni so nikajua tutakuwa wengi.
The guys were very quiet, yaani kama hawana midomo! Wakati tukiwa kwenye foleni mdogo wangu akanipigia simu, tukawa tunaongea about school fees za shule fulani hivi. Ile namaliza kuongea tumeshafika lapa Dawasco. Nikawauliza mbona hamjapakia abiria wengine? Wakadi usiku umeingia afu wanaogopa foleni. Hofu ikazidi sana ila nikajipa moyo kuwa Mungu atanilinda.
Tulipofika njiapanda ya Kilwa road, wakaingia barabara ya shimo la udongo kule Bandari na nilipowauliza wakadai wanakwepa foleni. Hapo sasa hofu ndo ilizidi sana. Nikapata wazo la kupiga simu home ila before that jamaa alokuwa uoande wa pili akanipokonya simu kisha wakafunga vioo na jamaa akanirukia uku nyuma nilipokuwa nimekaa. Alinikaba sana shingo mana nilikuwa nashindana nae, lengo ilikuwa ni kujaribu kumkamata sehemu fulani ili akose nguvu aniachie! Waapi!Kwani hata sehemu hizo nilifanikiwa kuzigus? Nahisi jamaa labda hana! Alinipa ngumi moja huku kanikaba na akapromise kuitoa roho yangu iwapo sitofanya fujo. Sikuwa na ujanja zaidi ya kutulia na ku surrender! Jamaa akaniambia wao wanataka hela na vitu vyote vya thamani nilivyokuwa navyo.
I had earrings and the chain (hazikuwa original) basi jamaa walivyo wajinga wakaona deal! Wakauliza thamani yake nikawaambia zote thamani yake ni laki 5!Wakajua bonge la deal! Alokuwa ana drive akaanza kumpigia mtu anamwambia anamletea mzigo (nikajua kabisaa mzigo ni mie, yaani natolewa kafara au ndo nabakwa kiroho mbaya). Sio siri nililia sana, nikawasihi waniachie nitawapa hata pesa kama wanataka mana account yangu benk ilikuwa inapumua kiasi chake! Wakachukuakila nilichokuwa nacho, cash, handbag, bank cards zangu zote yaani waliniacha sina ata kumi. Wakati huo jamaa kanishika shingo mikono yote miwili ili nisifurukute.
Akaniambia dada tumeshachukua chetu sa ivi tuntafta sehemu ya kukuacha na tukikushusha usigeuke nyuma mana tutakumaliza. Hapo mimi nikawa naomba Mungu waniache tu salama na kweli kufika sehemu wakasimamisha gari, mkabaji wangu akaniachia wakafungua mlango wakaanisukuma ila sikuambua chini. kweli sikugeuka nyuma nikaanza kukimbia kutafta msaada. Kichwani mwangu nilijua wamenipeleka mbali sana, ajabu nauliza watu pale wapi wananimbia maeneo ya Kanisa Katoliki Kurasini!!
Nilipiga magoti na kumshukuru Mungu, wasamaria wakanisaidia kutafta bodaboda, nikafika home na kwa vile I had money home basi nikamlipa bodaboda. Thats what happened to me, ni story ndefu ila napenda especially wadada wajifunze haya.
- Ni heri ukabanane kwenye daladala hata kama una pesa ya kupanda taxi kuliko ku risk maisha yako kuchukua taxi au private cars.
- Kama mtu humfahamu, hata kama atajifanya kumjua hadi baba yako, please do not trust them
- Ikitokea unalazimika kupanda a private car au taxi make sure uko na watu mnaofahamiana not strangers especially men, uwiiii!!
- Jenga utamaduni wa kunote plate numbers za gari lolote unalopanda iwe taxi au gari binafsi na ikibidi mtaarifu mtu/watu wa karibu ili in case of anything unaweza kupata msaada.
- Epuka sana kutoka job night hours kwa kisingizio cha kukwepa foleni na usumbufu wa magari. Ni heri usafiri mchana its safe than usiku.
- Dont entertain your employer aisee, mimi hili lilinitokea kwa sababu ya mwajiri wangu mana kulikuwa na kazi zilizonilazimu kuzifanya on that day! Fanya kazi kwa muda mliokubaliana kwenye contract tu na hata kama unalipwa overtime my dear usiendekeze sana pesa kwani hizo zintaftika ila uhai ukipotea hautaftiki.
- Tembea na silaha zetu za imani ama bible au msaafu mana kwa njia ya ajabu zaweza kukusaidia pale usipodhania wala kutegemea.
- Tumkumbuke sana Muumba wetu na tumtegemee in our daily life. Unapotoka asubuhi kuja kazini pray to him and ask for his protection. Huu uwe utamaduni wako daily
- Mhh, siku hizi kumuliki gari sio anasa, unaepusha kwa asilimia kubwa kupatwa na majanga kama haya. Baada ya kuumwa na nyoka sasa sioni kama kumiliki gari ni anasa, nimechukua hatua na wewe mwenzangu usiogope kuchukua hatua.
NOTE: Kuna watu walionilaumu na pia mtanilaumu kwamba I was stupid kwa kuchukua uamuzi wa kupanda hilo gari but kwangu mimi nafahamu kuwa everthing happens with reasons! Kwa namna moja au nyingine Mungu alitaka kunifundisha kitu mimi pamoja na wengine/wewe unaesoma huu uzi. Binadamu wengi siku hizi wamekuwa sio wema kabisa! Kuna tetesi kuwa wengine wanawateka watu na sio kwamba wanawapora ila wanawaua na kuwatoa kafara! Please be careful especially wadada mana sie ndo tupo kwenye risk coz we cant fight back.
0 comments:
Post a Comment