Friday, 16 August 2013

HUYU NDIYE MCHEZA MIELEKA ALIEJITANGAZA KUWA YEYE NI SHOGA.....!!!


Hii ni habari nyingine ya kuwaacha watu midomo wazi, na hii ni kufuatia hatua ya Nyota Mieleka kutoka WWE, Darren Young kuweka wazi kuwa yeye ni shoga.
Kutokana na tabia na mfumo wa Wanamieleka kuunda matukio ya kutengeneza ili kujipatia 'kiki', hapo awali hatua hii ya kujitangaza kwa Darren ilidhaniwa kuwa ni utani, lakini kimsingi imeonekana kuwa hakuna points zozote ambazo angeweza kujipatia kwa kujitangaza kuwa ni shoga.

Darren amesema kuwa anajivunia hali yake hii na yeye ni mtu mwenye furaha licha ya ma-shoga kuwa bado ni watu ambao jamii inawachukulia tofauti.

0 comments:

Post a Comment