Mwanamke mmoja wa huko New Hampshire USA
ameonja joto ya jiwe baada ya uwongo wake kuvaliwa njuga na Trafiki
aliyeifanya kazi yake zaidi ya kawaida. Mwana mama huyo aliondolewa
barabarani baana ya rada ya trafiki Cummings kunasa gari yake ikienda
mwendo wa 82 MPH wakati eneo lile lilitakiwa speed ya 65 MPH.
Baaya ya Trafiki Commings kushikilia
leseni yake, mwanamke huyo aliyeonekana katika hali ya majonzi
alimwambia trafiki kuwa ana baba yake hospitalini, anaugua kansa hatua
ya nne na kwamba mapigo yake yalikuwa yakipiga mara sita tu kwa dakika
hivyo alikuwa akiwahi kumwaga kabla hajafariki dunia. Kwa hali ya huzuni
aliyokuwa nayo trafiki Commings alimrudishia leseni yake haraka na
kumruhusu aende kumwaga baba yake kabla hajakata roho.
Hata hivyo, trafiki Christopher J.
Cummings aliamua kumuuliza amtajie jina la baba na hospitali aliylazwa,
mwanamama Williams bila kusita alitaja. Baadaye trafiki Commings alipiga
simu hospitalini kuuliza mgonjwa yule lakini aliambiwa hakuna mgonjwa
mwenye jina hilo pale hospitalini. Commings alifadhaaika sana kuona
kwamba binadamu anaweza kujiweka katika hisia za huzuni kiasi kile na
zaidi kudanganya kiasi kile. Trafiki Commings hakuishia hapo, aliamua
kuingia kwenye mtandao na kutafuta taarifa za Carley Williams, ndipo
alipogundua kuwa jina la baba yake alilitaja lilikuwa kwenye listi ya
watu waliokufa tangu mwaka 2008, kwamba baba yake alishafariki kitambo
lakini Carley akaamua kutumia jina hilo la marehemu kana kwamba bado
yuko hai na ndiyo anakaribia kukata roho. Afande yule anayefanya kazi
yake inavyostahili aliendelea kumpekua Carley kwenye mtandao na kugundua
pia kwamba gari lile alilokuwa akiendesha lilishafutiwa usajili.
Jumapili iliyopita Commings akamfuata
Carley nyumbani kwake na kumwonyesha cheti cha kifo cha baba yake,
Carley aliangalia chini kwa aibu lakini bado anaendelea kukataa kuwa
yule sio baba yake ila mjomba wake. Hata hivyo afande Commings
alimwambia kwamba hakumjia kwa kosa lile la udanganyifu ingawa
lilimuumiza sana, ila amekuja kumkamata kwa kosa la kuendesha gari
lililoondolewa kabisa kwenye usajili wa magari. Carley Williams
alipelekwa kituo cha polisi cha Nashua kwa kosa la kuendesha gari
lisilosajiliwa.
Trafiki Commings anasema kwamba
alishazoea kudanganywa na wavunja shera za barabarani na mambo mengine
alikuwa anayachukulia poa tu lakini hili la Carley limekuwa kubwa na
limemsumbua sana kichwa kuona ni kwa namna gani binadamu anaweza utumia
uongo tena unaohusisha marehemu kukwepa mkono wa sheria.
0 comments:
Post a Comment