Agosti
7, 1998

Mashambulio
ya kigaidi ya 7 Agosti 1998 katika Afrika ya Mashariki yalitokea katika miji ya Dar es salam
na Nairobi kwa
kulipusha malori yaliyojaa baruti mbele ya balozi za Marekani kila
mahali. Angalau watu 224 waliuawa na maelfu kujeruhiwa.
Watendaji
walikuwa raia wa nchi za Kenya na Tanzania pamoja na nchi za Kiarabu mbalimbali. Walitekeleza
mashambulio kwa maagizo ya kundi la Jihadi ya Kiislamu ya Misri ambalo ni
sehemu ya mtandao wa Al Qaida iliyoongozwa na Osama
bin Laden.
UBALOZI WA MAREKANI MJINI NAIROBI
Gaidi
wa pili Mohamed Rashed Daoud Al-Owhali alimtupia kombora ya mkononi lakini
alimkosea. Bwaku alifaulu kukimbia na kufikia kona ya jengo akajiokoa. Hapo
Azzam alianza kufyatua risasi hovyo. Hapo Al-Owhali alikimbia kuelekea mtaa wa
Haile Selassie akajiokoa wakati Azzam akajilipusha kwa baruti kwenye lori.
Mlipuko mkubwa ulitikisisha ubalozi na jengo jirani la Ufundi Building. Mshtuko
wa mlipuko uliharibu pia vyoo vya madirisha katika kipenyo cha kilomita 1 na
sauti yake ilisikika kwa umbali wa kilomita 16.
Jengo
la ubalozi liliharibiwa kiasi tu kwa jumla likasimama kwa sababu lilijengwa
imara. Ndani ya ubalozi walikufa watu 44, Wamarekani 12 na wafanyakazi wengine
32, wengi wao Wakenya hasa kama waliathiriwa na mshtuko ulioingia madirishani
na kuangusha kuta za ndani.
Vifo
vingi vilitokea kwa sababu jengo dogo jirani la Ufundi building libomolewa
kabisa na kuanguka. Wahanga wengi walikuwa vijana wanafunzi waliosoma kwenye
chuo cha ukarani ndani ya jengo hili pamoja na walimu na wafanyakazi wake.
Pamoja
na watu waliojeruhiwa katika majengo ya karibu sana kuna wengi waliouawa na
kujeruhiwa kwenye barabara ya Haile Selassie kwa sababu moto na mshtuko wa bomu
zilielekezwa kati ya kuta za ubalozi na Ufundi Building. Basi iliyokwama kwenye
msongamano wa magari mbele ya kiingilio cha ubalozi ilichomwa kabisa pamoja na
abiria zake.
Watu
wengi walijeruhiwa macho kwa vipande vya kioo; walisikia mlipuko wa kwanza wa
kombora la mkononi na risasi zilizofyatuliwa a Azzam wakaenda madirishani
kuangalia kuna nini wakapigwa vipande vya kioo cha madirisha usoni wakati bomu
ililipuka.
Karibu
kwenye dakika ya mlipuko wa Nairobi shambulio la pili lilitokea kwenye ubalozi
wa Marekani mjini Dar es Salaam. Hata hapa dereva alijaribu kuingia kwenye eneo
la ubalozi kwa lori lakini alikataliwa getini akalipusha mzigo wake. Hapa ni
watu 11 waliokufa na 85 waliojeruhiwa. Idadi ya wahenga ilikuwa ndogo kuliko
Nairobi kwa sababu ubalozi ulikuwepo nje ya kitovu cha jiji kando la mtaa wa
Bagamoyo na nafasi likuwa kubwa hadi majengo ya jirani.
Mwaka
uleule washiriki wa kwanza wa mashambulio haya walikamatwa na kukabidhiwa kwa
Marekani. Hadi mwaka 2010 watu 5 walihukumiwa jela ya maisha kwa kushiriki
katika ugaidi wa 7 Agosti.
0 comments:
Post a Comment