Watalii wakiendelea kutazama simba hao wenye uchu. |
Ni karibu kuliko watu walio wengi wangeweza kutamani kuingia kwenye kundi la simba wenye njaa.
Lakini boma hili linalotembea huruhusu watembeleaji kwenye hifadhi ya Orana Wildlife Park, huko Christchurch, New Zealand, kutazamana ana kwa ana na simba hao ... wakati wa muda wa malisho.
Watalii hadi 20 hulipa Pauni za Uingereza 15 kila mmoja kujibana kwenye kizimba hicho pamoja na walinzi na kutazama simba hao wakiwa wanalishwa.
Simba huruka kila upande na juu ya boma hilo linalotembea lililozungushiwa wavu kuruhusu watu kusogea karibu inavyowezekana kwa usalama dhidi ya wanyama hao hatari.
Walinzi huwalisha simba hao kutokea ndani ya kizimba hicho, hivyo kuwapa wageni nafasi ya kuwatazama wakilishwa kwenye makazi yao.
Msemaji wa mbuga hiyo, Nathan Hawke, alisema: "Boma hilo la Simba ni pekee ya kawaida kwa wageni.
"Huku watu wakiwa wanaweza kuona simba kwenye maeneo mengi tofauti, tunafikiri tunaweza kukufikisha karibu ambavyo ungependa kiusalama kutaka kuweza kutazama wanyama hawa wa aina yake.
"Tumekuwa na wageni ambao wamekuja tu Christchurch kujumuika kwenye boma hili.
"Ni njia ya kuvutia kuwaonyesha simba na pia kutuwezesha kujadili njia gani ambazo wageni wanaweza kumsaidia Mfalme huyo wa Nyika."
Safari za kila siku kwenye malisho hayo ya simba ndani ya boma hugharimu Dola za Marekani 30 (Pauni 15) kila mmoja, huku kimo cha mwisho kikiwa ni mita 1.4 kwa sababu za kiusalama.
Orana Wildlife Park ni hifadhi pekee ya wazi nchini New Zealand, ikiwa na ukubwa wa hekta 80 za ardhi inayofanana na eneo la mbuga.
Zaidi ya wanyama 400 kutoka aina tofauti 70 hupatikana ndani ya hifadhi hiyo.
0 comments:
Post a Comment