Nembo silaha za Biologia.
Dalili za muathirika wa gesi za zumu akitokwa na mapovu puani
Dalili za muathirika wa gesi za sumu alishindwa kupumua na hatimaye kuvuja damu puani na mdomoni
Mtoto akipatiwa huduma ya kwanza akisaidiwa kupumua
Kutokana na gesi ya sumu kushambulia mfumo wa upumuaji, watoto huathirika haraka zaidi ndiyo maana watoto wengi walikufa Syria
Waathirika wa sumu ya gesi Syria wakizikwa katika kaburi la pamoja
Waziri wa mambo ya nje wa
Uturuki Ahmet Davutoglu leo amethibitisha kwamba nchi yake itaungana na
vikosi vya kimataifa kuishambulia Syria hata kama Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa halitafikia muafaka wa pamoja.
Kwa sasa hali ya mambo nchini Syria inaweza kubadilika muda wowote kutokana na Serikali ya Bashar Asaad kutuhumiwa kuwauwa wapinzani wake kwa gesi ya sumu ( Chemical Wepons) Alhamisi iliyopita ilishuhudiwa watu zaidi ya 1,300 wakiuwawa kwa sumu hiyo.
Awali Rais Obama wa Marekani ambaye anaonekana kukwepa kwa nguvu zote kujiingiza katika mzozo wa Syria, alikuwa amesema kama Asad atatumia mabomu ya sumu masi atakuwa amevuka "red line" na marekani haitakuwa na budi kuingilia kati mzozo huo. Hata hivyo rais huyo wa marekani anaendelea kushinikizwa na wapinzani wake kuchukua hatua kali dhidi ya Syria. Ufaransa nayo imesema iko tayari kufanya mashambulizi dhidi ya serikali ya Asad. Hata hivyo, Umoja wa Mataifa umetuma waangalizi wa kuchunguza kama kweli mabomu ya biologia yalitumika kuuwa watu kabla baraza la usalama la umoja wa mataifa halijaridhia adhabu dhidi ya Syria.
Syria inaungwa mkono na Iran na wanamgambo wa Hesbollah pamoja na kupewa silaha kutoka Urusi. uchina pia ni rafiki wa Asad hivyo shinikizo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaweza kukosa nguvu kama Urusi na China ambao ni wanachama a kudumu wa Baraza hilo wataamua kutumia kura ya turufu.
Mzozo wa Syria ambao umedumu kwa zaidi ya miaka miwili ulianza na vuguvugu la mapinduzi ya kiraiya yaliyoitwa (Arab Spring) yalianzia Tunisia, Misri, Libya,Syria na nchi nyingine za kiarabu ambapo kila yalipotokea yaliacha makovu makubwa na kubadili historia ya nchi husika moja kwa moja.
Kuishambuliana hatimaye kuiangusha Serikali ya Asad inazidi kuwa ni jambo lisiloepukika kutokana na mataifa ya magharibi na Israel kuogopa silaha alizo nazo Asad ya Bialogia zisije zikaangukia mikononi mwa Hesbillah au mikononi mwa Alquaida.
0 comments:
Post a Comment