Miss World 2013, Megan Young. |
Mshindi wa Pili Miss World 2013, Marine Lorphelin. |
Mshindi wa Tatu 2013, Carranzar Naa Okailey Shooter. |
Wakati mrembo kutoka Philippines,
Megan Young akiibuka kidedea Shindano la Miss World 2013, mrembo kutoka
Afrika, Miss Ghana Carranzar Naa Okailey Shooter amechomoza kati ya
warembo 130 na kushika nafasi ya tatu.
Megan amerithi taji hilo kutoka kwa mrembo wa China, Yu Wenxia aliyefanya hivyo mwaka jana.
Katika shindano hilo lililofanyika mjini Jakarta, Indonesia na kumalizika muda mfupi uliopita, mrembo kutoka Ufaransa, Marine Lorphelin alishika nafasi ya tatu.
Tanzania kama kawaida yake, haikuweza kabisa kufua dafu baada ya mshiriki wake, Brigitte Lyimo kushindwa kufurukuta katika mtanange huo mkali na unaobeba hisia kubwa miongoni mwa wadau wake duniani kote.
Dalili za Miss Ghana kung'ara katika shindano hilo zilizidi kuongezeka hasa kutokana na umahiri wake katika kujibu swali na kujiamini.
0 comments:
Post a Comment