Serikali imetangaza kuyafungia
magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia Septemba 27, mwaka huu kwa
kuandika na kuchapisha habari na makala za uchochezi.
Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kuchapishwa kwa siku 14, wakati MTANZANIA limefungiwa kwa siku 90.
Hatua hiyo imetangazwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo.
Kwa mujibu wa Mwambene, adhabu hiyo kwa gazeti la MWANANCHI imetangazwa katika tangazo la Serikali namba 333 la tarehe 27 Septemba, 2013 na kwa upande wa MTANZANIA imetangazwa katika tangazo ya Serikali 332 la tarehe 27 Septemba, 2013.
Mwambene alitumia nafasi hiyo kutaja habari hizo kuwa ni pamoja na ile iliyosema: "Mishahara Mipya Serikalini 2013 kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kuchapishwa katika vyombo vya habari".
Kwa mujibu wa Mwambene waraka huo ulikuwa wa siri ambao haukupaswa kuchapishwa magazetini.
Mwambene alisisitiza kwa Wahariri na waandishi wa habari kuzingatia weledi na miiko ya taaluma zao.
0 comments:
Post a Comment