Tuesday, 1 October 2013

MFADHILI WA AL-SHABAAB KENYA ASEMA BAADA YA WESTGATE, SASA NI UINGEREZA...

  

Abubaker Shariff Ahmed 'Makaburi' wakati wa mahojiano juzi.
Mhubiri kisirani anayetafutwa kwa kuajiri wauaji kwenye kundi ambalo liliua mamia ya wananchi katika jengo la Westgate Shopping Mall mjini Nairobi ametahadharisha jana kwamba Uingereza ilikuwa kusudio linalofuata.

Abubaker Shariff Ahmed, ambaye anafahamika kwa wafuasi wake kwa jina la Makaburi, alisema magaidi wanapanga kuua Waingereza wasio na hatia katika mpango wao wa kulazimisha sheria ya Sharia duniani kote.
Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na gazeti la Daily Mail, alimtaja David Cameron kama mlengwa mkuu kwa kundi hilo la magaidi wa Al-Shabaab, ambalo lilishambulia kituo cha biashara cha Westgate Mall mjini Nairobi, kenya, Jumamosi iliyopita.
Alipoulizwa kama ugaidi utafanyika nchini Uingereza, Makaburi alisema: "Ndio. Waingereza watakuwa walengwa wakuu binafsi. Hiyo inamaanisha watalii katika mitaa watauawa. Wote mtakufa.
"Waingereza wataangamizwa. Marais wenu na mabaraza yenu ya mawaziri, wana hatia. Obama ni muuaji mkubwa. Ninajitolea maisha yangu kwa ajili ya kifo chake.
"Kama ilivyo kwa David Cameron. Ndio, lazima wauawe."
Madai ya Makaburi yamekuja huku Cameron akifichua aliamuru walinzi na maofisa usalama wa taifa kusuka mipango kukabiliana na mashambulio ya kigaidi kwenye vituo vya kibiashara vya Uingereza.
Waziri Mkuu huyo, ambaye aliongoza mikutano ya kamati ya majanga ya Cobra wiki iliyopita, alisema hakuwa na akili ya mipango kwa mashamulizi ya 'karibu mno' nchini Uingereza.
Lakini alipoulizwa kama alikuwa akifahamu kwamba Waingereza wenye asili ya Kisomali wanaweza  kupeleka ugaidi nchini Uingereza, Cameron alisema:
Kwa namna ya kushangaza, Makaburi bado hajahojiwa na maofisa nchini Kenya kuhusiana na shambulio hilo la Westgate, licha ya kutuhumiwa na Umoja wa Mataifa kuwa 'mwezeshaji mkuu na mwajiri' wa magaidi vijana katika eneo hilo.
Huku akisemekana kumwajiri 'Mjane Mweupe' Samantha Lewthwaite kwenye kundi hilo, alisisitiza juzi kwamba hafahamu mwanamke huyo aliko au kama alihusika katika utekaji nyara wa hivi karibuni.
Akimwelezea Samantha, mwenye miaka 29, kutoka Aylesbury, Buckinghamshire, Makaburi alisema: "Ninamwita Samantha Fox. Yeye ni mjanja. Hatufahamu lolote kuhusu yeye. Hayupo. Kama ni kweli basi ni mwanamke wa shoka."
Samantha, mama wa watoto wanne, ni mjane wa mlipuaji wa London Jermaine Lindsay na amekuwa mafichoni katika Afrika Mashariki.
Ni mwanamke anayetafutwa zaidi duniani baada ya Interpol kutoa hati ya kukamatwa duniani kote wiki iliyopita.
Juzi, Makaburi, mwenye miaka 50, alikuwa amejificha katika kitongoji kimoja kwenye kisiwa cha Mombasa nchini Kenya. Anaishi kwenye makazi binafsi, amegoma kuondoka hata kwa sala kwa hofu ya kuuawa.
Anatuhumiwa kuwa sehemu ya mtandao ambao unaelekeza karibu magaidi 100 wa Kiingereza katika kambi za Afrika Mashariki.
Alionya kwamba utekaji wa Westgate ulikuwa mwanzo tu wa mfululizo wa mashambulizi ya kulipa kisasi kwa nchi za Magharibi kuingilia nchi za Kiislamu.
"Imeamuliwa," alisema. "Kama siwezi kuishi na familia, kwanini Waingereza waweze kuishi na familia zao?"
Alipoulizwa anajishughulisha na nini akiwa mafichoni, alijibu kwa mzaha: "Ninaandaa bomu."

0 comments:

Post a Comment