Bibi Titi na Mwalimu wakihutubia wananchi enzi za TANU.
WIKI iliyopita niliandika juu ya kesi ya uhaini iliyoanza kunguruma Juni 8, 1970 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar.
Niliwataja pia baadhi ya watuhumiwa waliofikishwa mahakamani lakini
mtuhumiwa mmoja alishangaza wengi na si mwingine isipokuwa ni Bibi Titi
Mohammed (45).
Wengi walishangaa na kujiuliza, mama huyu kweli alitaka kumuua Rais
Julius Nyerere? Walijiuliza hivyo kwa sababu enzi hizo mwanamke
kujihusisha na kitu kizito kama hicho ilikuwa ni ndoto, lakini yeye
alifanya na alimwaga fedha kwa kazi hiyo.
Lakini pia wananchi walishangaa kwa kuwa Bibi Titi aliwahi kuwa waziri na rais wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT).
Kama ilivyo kwa watuhumiwa wengine ambao walikuwa na majina bandia ya
‘kazi’. Mama huyo naye mahakama iliambiwa alikuwa na majina mengine
aliyojiita au kuitwa nayo ambayo ni Mama Mkuu, Mwamba au Anti wakati wa
mipango yao ya mauaji na kuipindua serikali ya Nyerere.
Bibi Titi aliyezaliwa mwaka 1926 alikuwa kivutio kila alipokuwa
anafikishwa mahakamani kwani wakati wa ujana wake alikuwa mtu wa karibu
wa Nyerere.
Alishirikiana wakati wa kudai uhuru na hata baada ya taifa kuwa huru.
Ilielezwa kuwa Bibi Titi aliunganishwa kwa Nyerere na dereva mmoja wa
teksi ya nyumbani kwao mwaka 1954 na akawa mmoja wa waanzilishi wa
chama cha Tanu.
Biti Titi alikamatwa na polisi Oktoba 1969 akiwa na waziri wa zamani wa
kazi, Michael Kamaliza pamoja na maofisa wanne wa JWTZ na wote
wakafunguliwa mashitaka ya kutaka kumuua na kumpindua Nyerere.
Ushahidi mwingi ulitolewa mahakamani na ilielezwa kuwa alikuwa akimwaga
fedha ili kufanikisha mpango huo haramu kutokana na ufadhili wa mtu
mmoja ambaye alikuwa nje ya nchi.
Je, nani alikuwa akimpa fedha? Utapata majibu haya katika toleo lijalo.
GPL
0 comments:
Post a Comment