Nyota wa tasnia ya filamu , Jaqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amedai kuwa hawapendi sana wanaume wenye fedha kwani wengi wao ni waume za watu...
Wolper anadai kuwa nao si rahisi kuonyeshwa mapenzi yao ya dhati kwani mapenzi yao ni ya chumbani tu...
" Unajua
unapokuwa na mtu mwenye fedha zake , alafu mtu mzima, ni lazmia ukose penzi la
kweli kwani mapenzi yenu ni chumbani tu, hamuwezi kutembea pamoja kukaa
kama vile ni wapenzi ...
"Lakini ukiwa na kijana ambaye hana pesa
na wewe una kazi lazima akuonyeshe jinsi mapenzi yalivyo kwa kukuweka
karibu kimahaba na wewe ukafaidi penzi kutoka kwake..
“Wanaume wengi wenye pesa zao huniona nina dharau, lakini mimi ni
binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke .
"Kuna watu wanaamini pesa zao ndio kila kitu,
kiukweli kwangu siyo hivyo , ukileta mapenzi hayo lazima unione nina
dharau”,anasema Wolper Gambe.
Wolper anadai kuwa kuna watu ambao huwanyooshea vidole wasanii maarufu kama yeye kwa
kuwaona kama vile ni Malaya lakini wanasahau kama nao ni binadamu na
wanaroho kama wanadamu wengine....
Jack Wolper anasema wao si malaika , wanapenda na kupendwa, kwa
hiyo ukimuona ana kijana Serengeti boy ujue ni kwa ajili ya kupata
penzi nzito na kusikilizwa haja zake.
0 comments:
Post a Comment