?"
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba amesema bungeni leo kwamba Chadema ilipanga kufanya shambulio la bomu kwenye mkutano wa Soweto jijini Arusha.
Amesema hakuna jambo ambalo Chadema wamewahi kupanga wakashindwa.
“Itakuaje mtu amechukua mkanda wa tukio la umwagaji wa damu bila kutikisika au mchukuaji kukimbia, haiwezekani- hiyo walipanga.
“Inakuaje amechukua mkanda wa video kama mkanda wa harusi, yaani kama mkanda wa sendoff.? Amehoji Mwigulu huku wabunge wa CCM wakimuunga mkono kwa kupiga meza bungeni.
Mapema wiki hii katika mkutano wa Chadema, mtu mmoja asiyefahamika alirusha bomu kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha watu wanne kufariki dunia na wengine 68 kujeruhiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mt Meru, Arusha.
0 comments:
Post a Comment