*WAPORAJI WASHINDWA KULIENDESHA
WALITELEKEZA
*BINTI YAKE ALITEKWA MWEZI MEI KWA GARI
HILO HILO
Mwanamke aliyefahamika
kwa jina la Melissa Torrez ameuacha umma midomo wazi baada ya kulipata gari
lake lililopotea kwa kutumia akaunti ya Facebook.
UKISTAAJABU YA MUSA, UTAYAONA YA
FIRAUNI …….
Melissa
Torez mwezi Mei mwaka huu alikutwa na masahibu ya binti yake kutekwa na mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la David Hernandez ambaye alikamatwa na kuhukumiwa
kwa makosa ya utekaji.
Julai 23
mwaka huu akiwa Albuqueque jatika Jimbo la New Mexico nchini Marekani aliibiwa
gari lake aina ya Chrysler 300.
Baada ya
kupatikana kwa taarifa hizo mwanamke huyo alikaa kitako namna gani atakavyoweza
kulipata gari lake hilo la thamani ndipo alipoamua kuchukua picha ya gari hilo
na kulitupia katika Ukurusa wa FACEBOOK ambao ndugu, jamaa na marafiki
walichangia katika habari hiyo “post” na ndipo Polisi walipoweza kulipata
kirahisi kabisa siku iliyofuata.
Akizungumza
na KOB Eyewitness News 4, Mellisa alisema wakati anaondoka katika eneo la
kuegeshea magari usiku wa siku hiyo akiwa na rafiki zake walitokea wanaume 3
waliowashurutisha watoe pochi zao “vipima joto”, simu na funguo ya gari hilo
ambalo walikuja nalo akiwa na marafiki zake.
Baada ya
tukio hilo mmoja wa rafiki zake alimwambia kwamba mambo yatakwenda sawa kabisa
bila wasiwasi ndipo alipomuuliza itawezekanaje kwenda sawasawa wakati shimo la
kutolea risasi lilipoelekezwa kwao.
Torrez
alitupia picha hiyo katika ukurasa wa FB na picha ya gari lake la Chrysler 300
ndipo mmoja wa rafiki zake aliyefahamika kwa jina la Enrique Venerio katika
ukurasa wa FB alichukua na kuipeleka polisi huku kazi ikiendelea Torrez
aliwaambia rafiki zake kupitia mtando huo wa kijamii kuhus mkasa huo.
Pia kwa
majirani wenzake waliokuwa wakiishi kutoka Santa Fe hadi Grants katika Jimbo
hilo hilo la New Mexico nchini Marekani.
Polisi ya
eneo la Albuquerque walipata taarifa na picha ya gari lenyewe na msako wa
kulipata gari hilo.
Venerio alikuwa
miongoni mwa watu waliomsaidia mwanadada Melissa kulitafuta gari hilo usiku
kucha bila mafanikio.
Baada ya
uchunguzi wa Polisi siku iliyofuata waligundua kuwa waporaji wale
walilitelekeza gari lile umbali si mrefu kutoka kwenye eneo la tukio kutokana
na ukweli kwamba walishindwa kuliendesha.
Polisi
imesema walilikuta gari hilo lakini waporaji hao ambao walifanya uhalifu huo
wakiliacha lilikiwa pekee yake na funguo zake huku pesa, simu, vipima joto.
Itakumbukwa
kwamba mwezi Mei binti yake alitekwa kwenye gari hilo hilo la Chrysler 300.
CHANZO: YAHOO
NEWS/KOB Eyewitness News 4
0 comments:
Post a Comment