*ASTRONAUTS AMSTRONG NA ALDRIN, BINADAMU WA KWANZA KUFIKA
MWEZINI
*ASTRONAUTS NEIL AMSTRONG NA EDWIN ALDRIN WALISOMEWA DUA YA
KIFO
Rais pekee wa Marekani tangu kuanzishwa kwa taifa hilo mwaka
1776 aliyejiuzulu Richard Nixon alifanya kitu ambacho hakikutegemewa na wengi
endapo kilikuwa kimepangwa ama la.
UKISTAAJABU YA MUSA , UTAYAONA YA FIRAUNI…..
Ilikuwa Julai 20, 1969 ambapo
binadamu wa kwanza walitua mwezini. Chombo kiitwacho US Apoll 11 kiliwabeba
wanaanga wa Marekani Neil Amstrong na
Buzz Aldrin kufika kwenye uso wa mwezi na kuikanyaga ardhi yake.
Baada ya kumaliza kulichowapeleka
huko walirudi salama huku dunia hususani nchini kwao.
Lakini ukweli ni kwamba wakati
wanaenda mwezini jamii ya Wamarekani hawakutegemea kama wangeweza kurudi salama
kutoka katika anga za mbali.
Rais Richard Nixon alikuwa ni rais
wa 37 wa Marekani aliyetawala kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1969 hadi 1974,
ambaye naye alikuwa miongoni mwa Wamarekani ambao waliamini wapendwa wao
wasingweza kurudi.
Rais Nixon aliaandaa hotuba yenye ukurasa 1.5 kwa ajili ya
kuomboleza vifo vyao endapo US Apollo 11 kingeshindwa kurudi duniani.
Katika Hotuba yake Rais Nixon
aliandika Julai 18, 1969 kwa kuwaelezea Wanaanga hao wawili kuwa waliyatoa maisha yao kwa
ajili ya kutafuta kweli kwa manufaa ya taifa
hivyo tunatambua hao ni mashujaa. Na kwamba wote (yaani wamarekani) wautazame
Mwezi na kuwakumbuka Armstrong na Aldrin kwa kujitoa kwao.
Na kwamba baada ya kituo cha mawasiliano
ya Anga (NASA) watakapomaliza mawasiliano na Wanaanga wenzao basi, viongozi wa
dini watafuata kwa hatua za kidini za kufanya mazishi pembezoni mwa bahari.
Rais Nixon alifariki akiwa na umri
wa miaka 81 Aprili 22, 1994, wakati Neil Amstrong aliaga dunia akiwa na umri wa
miaka 82.
Buzz Aldrin bado yu hai hata leo
akiwa na umri wa miaka 83 , akiishi na familia yake.
Wanaanga hao walikanyaga ardhi ya
mwezi saa 3:15:16 (UTC), sawa kabisa na saa 8:15:16 mchana (EAT).
CHANZO: MANDATORY.com/
OMG Facts
0 comments:
Post a Comment