KLABU ya Al Markhiya Sports Club ya Doha,
Qatar, imetuma barua kwa uongozi wa Simba ukiomba umruhusu kiungo wake Mwinyi
Kazimoto kujiunga na timu hiyo baada ya nyota kufanya vizuri katika majaribia
yake hivi karibuni.
Habari
za uhakika zinasema Kazimoto aliyekwenda Qatar wiki iliyopita kusaka nafasi ya
kucheza soka la kulipwa katika klabu hiyo, ameshafanyiwa vipimo vyote hivyo
kinachotakiwa ni kibali tu kwa ajili ya kuichezea timu hiyo iliyoasisiwa mwaka
1995 ambayo sasa inacheza Ligi Daraja la Pili.
Japo
nyota huyo aliondoka bila idhini ya viongozi wa Simba wala wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) kutokana na kuondoka nchini akitokea kambi ya timu ya taifa
ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Al Markhiya imeiangukia Simba kuomba
ridhaa yake.
Kiongozi
mmoja wa Simba alikiri kuwepo kwa barua hiyo iliyoandikwa na Mohamed Abu Ali,
lakini wenye mamlaka juu ya uamuzi huo ni viongozi wa juu wa klabu.
“Kweli
kuna hilo jambo, lakini siwezi kulizungumzia kwa undani zaidi kwani sina uamuzi
juu ya hili na hasa ikizingatiwa mazingira ambayo mchezaji mwenyewe aliondoka;
sasa tuwaachie viongozi wenye mamlaka,” alisema.
Hata
hivyo hakuna kiongozi yeyote wa juu wa Simba aliyeweza kupatika jana
baada ya kutopokea simu zao za viganjani.
Kama
Kazimoto atapata baraka kutoka kwa uongozi wa Simba atakuwa ni miongoni mwa
nyota wa Tanzania wanaopata ulaji wa kutakata kupitia soka la kulipwa.
CHANZO: TANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment