Bobbi Kristina (kulia) akiwa na mchumba wake, Nick Gordon. |
Binti wa Whitney Houston, Bobbi Kristina Brown ametangaza rasmi kwamba amechumbiwa.
Na mwanaume aliyebahatika, kama ambavyo wengi walitarajia, ni Nick Gordon, mtu ambaye Whitney alimkuza kwake kama mtoto wake wa kumzaa, ambaye amekuwa akielezewa kama 'kaka' wa binti huyo mwenye umri wa miaka 20.
Inamaanisha kwamba mbali na kusherehekea habari zake, Bobbi amejinasua kutoka kwenye mitego kujilinda.
Uhusiano wao umesababisha uchunguzi makini na muda wa kutosha wa kutungua macho yangu mama yao alipofariki dunia Februari mwaka jana.
Na hivyo Bobbi anakabili skendo hilo kwa kutuma taarifa mbalimbali kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Anaandika: "NDIO, mimi na Nick tumevishana pete. Nimechoka kusikiliza watu wakisema 'umechumbiwa na kaka yako au kama Whitney angekuwa hai tungekuwa pamoja au angeidhinisha hili."
"Wacha niweke sawa kitu fulani, sisi sio kaka na dada wa ukweli wala kaka yangu aliyeasiliwa. Mama yangu hakuwahi kumuasili. Isitoshe, mama alikuwa wa kwanza kusema kwamba alifahamu kwamba tunaelekea kuwa wapenzi. Mama yangu ananifahamu vema kuliko yeyote kati yenu."
"Watu wanahitaji kuacha kabisa kuhukumu uhusiano wetu. Kwa hakika kabisa ni uamuzi wangu mie mwenyewe nani nataka kuwa naye.
"Ndiyo, uhusiano wangu hauwezi kuwa bila mapungufu. Tutakuwa na migongano ya hapa na pale, kama ulivyo uhusiano mwingine wowote.
"Na tumewahi kuwa na migongano yetu. Unaweza au kutoweza kukubaliana na uhusiano wetu. Unaweza au kutoweza kuuheshimu. Nihukumuni, endeleeni.
"Maoni yenu ni yenu na yangu ni yangu. Ni maisha yangu na si yenu. Uamuzi ninaofanya hauwahusu. Usiku mwema!"
0 comments:
Post a Comment