Elizabeth Surrey. |
Ofisa Magereza wa kike anayetuhumiwa kwa kuwa na mahusiano yasiyoruhusiwa na mfungwa amefikishwa mahakamani.
Elizabeth Surrey, mwenye miaka 25, kutoka Chelmsford, Essex, anatuhumiwa kwa mwenendo mbaya kwenye ofisi ya umma baada ya madai kuibuliwa kuhusu tabia yake wakati akifanya kazi kwenye gereza la HMP Chelmsford kati ya Machi 11 na Aprili 5.
Mashitaka hayo yanahusiana na madai kwamba alituma kadi, barua na baruapepe kwa mfungwa aliyekuwa akitumikia adhabu, kupokea simu binafsi kutoka kwa mfungwa huyo, akimwonesha mfungwa huyo mpasuo wake na kuondoa kitambulisho chake kutoka Daraja B la jela na kushindwa kukirejesha.
Alifikishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi jana asubuhi lakini hakutakiwa kujibu chochote.
Surrey, ambaye amesimamishwa kazi, alizungumza tu kuthibitisha jina lake na anwani.
Aliachiwa kwa dhamana isiyo na masharti hadi tarehe nyingine ya kusikilizwa shauri hilo kwenye Mahakama ya Chelmsford mnamo Septemba 16.
HMP Chelmsford ni gereza la wanaume la Daraja B na taasisi ya wahalifu wenye umri mdogo.
Gereza hilo lilianza kama jela ya eneo hilo mwaka 1830 lakini baadaye likageuzwa kuwa gereza la Daraja B, jela ya watoto na gereza la eneo hilo tangu mwaka 1987.
Lilipanuliwa mwaka 1996 kupunguza msongamano lakini Januari Wizara ya Sheria ilitangaza sehemu ya gereza hilo itafungwa.
Uamuzi huo ulimaanisha kutakuwapo na upunguzwaji sehemu 132 kwenye eneo hilo.
Inspekta Mkuu wa Magereza aliishutumu menejimenti ya gereza hilo mwaka 1999 baada ya kugundua wafanyakazi walikuwa wakishindwa kuitikia kwa wakati ving'ora vya selo.
Mnamo 2005 hatahivyo, Chelmsford ilipongezwa kwa kuboresha viwango na taratibu kwa wafungwa.
0 comments:
Post a Comment