Kitu cha kuvutia kuhusiana na filamu hii ni uhusika wa mwigizaji maarufu kutoka Marekani, Idris Elba ambaye amevaa uhusika mkuu wa filamu hii kwa kucheza kama Mandela, na filamu hii mbali na kugusia harakati, pia inagusia maisha ya binafsi ya kiongozi huyu ikiwepo mahusiano yake na Winnie ambaye ni mtalaka wake.
Filamu hii imeongozwa na wongoza filamu maarufu Justin Chadwick, na itakuwa ni moja kati ya filamu kadhaa ambazo tayari zimekwishafanyika kuonyesha maisha ya Mandela ambaye kwa mujibu wa taarifa, amekwishatoa baraka zote kwa timu nzima inayoitengeneza kazi hii.
0 comments:
Post a Comment