Kuna hali
ambayo ukiwa nayo wewe binafsi utajihisi kuwa haupo sawa. Hali hiyo ni ya kawaida
kwasababu inamkuta kila mtu, kuna siku utakuwa mwenye furaha na amani na siku
ningine mwenye kujisikia vibaya kama mtu aliyepungukiwa na kitu fulani. Siwezi
sema unajiona kama mkosaji wa kila kitu, hapana. Bali unakuwa kama ‘’Mtu Mwenye
Kujikataa Mwenyewe Kwa Kila Jambo Unalofanya.”
Hizi ni
hisia ambazo ukiwa nazo utakuwa wewe binafsi huzipendi na kujijua kabisa haupo
sawa ila ni msukumo wa ndani yako ndio unakufanya uwe hivyo. Kwa maana nyingine
hii ni hali ambayo unaweza kuijenga au kuipinga.
Ni sawa kuwa
hivyo, huh…huwezi kuwa mwenye ‘’GOOD MOOD’’ wakati wote na ndio maana
tunakasirika pale tunapokosewa kwa kuwa sio wakati wote mambo yatakuwa vizuri.
Lakini ikiwa utakuwa katika hali kama nitakazozioredhesha hapo chini basi utahitaji
kubadilika. Hakuna kitu kizuri kama kujua udhaifu wako na kujijenga, jitahidi
kutorudia kufanya makosa ya mapungufu yako ya jana. Siku ya leo ni LEO fanya
mambo mazuri na makubwa kwa kadri utakavyoweza hivi ndivyo namna ya kujitambua na kujijenga. Fanya
hivyo kwa wiki, mwezi kisha fanya tathmini. Inamchukua mtu siku 21
(wiki 3) mpaka mwezi mmoja kubadilisha tabia. Jaribu leo kubadilika
kitabia na ninaamini baada ya muda huo niliotaja utanipa majibu kuwa
umeweza kubadilika na kuwa tofauti na hapo awali.
1. Unakuwa
na mawazo mengi, mengine hukutaka hata kuyafikiria badala ya kuwa hapa kimawazo.
-Unaweza
kuwa unaongea na mwenzako, unajikuta umehama kimawazo na kufikiria mambo
mengine badala ya kumsikiliza vizuri na kuwa hapo kwa wakati huo. Jitahidi
kufuata msemo huu ‘’Wherever You’re Be There’’. Ni muhimu muhimu uwe makini kusikiliza na kuonyesha uwepo wako kikamilifu mahali popote utakapokuwa.
2. Unajihisi
kupinga kitu chochote utakachoambiwa na mtu mwingine na kutaka kushindana hata
kama huna sababu ya kufanya hivyo.
-Hii
ni hali
ya kuwa hutaki kushindwa jambo lolote unaloelezwa hata kama unajijua
haupo
sahihi. Katika hali kama hii ni heri ukawa mpole na kimya kuliko
kuonekana mbishi au mtu usiyeambilika. Kama ukipigiwa simu ukiwa bado
upo katika hali mbaya (bad mood) ni bora usipokee na kama unamazungumzo
muhimu na mtu ni bora uhairishe mpaka siku nyingine utakapokuwa vizuri
kuliko kuharibu mambo.
3. Unaona
mahusiano yako na mtu fulani kwa namna moja au nyingine yanakukwaza katika
maisha yako.
-Inaweza
kuwa ni mpenzi wako, rafiki au jamaa yako kweli anakukwamisha katika
mambo yako. Cha kufanya hapo ni kupima ni kwa kiasi gani anakukwaza? Je
anaweza kubadilika utakapomueleza na kumpa muda wa kujirekebisha? Je
unaweza kumvumilia? Kumbuka hata wewe unaweza kuwa na hali ya kujisikia
huhitaji mtu kwa wakati huo hivyo nawe ukawa ni sababu ya kumchukulia
mtu vibaya. Ukijikuta upo katika hali hii ni bora utulie na kutafakari
kwa ufasaha. Don't Make A Permanent Decision Because Of Your Temporary Situation. Usivunje mahusiano bila kutathmini sababu ya wewe kufanya hivyo. Kuwa na marafiki wazuri ni lulu usiwaache waende.
4. Unajihisi
kukereka kupita kiasi kwa kila jambo unaloona halipo sawa.
-Ulishawahi
kuona mtu anachukia chochote kilichopo mbele yake? Mfano: Dereva
wa gari au
pikipiki anagombana na kila mtu anayekatiza barabarani au kukasirika
kila anapokutana na shimo au kikwazo chochote njiani. Kama ukiwa katika
hali kama hiyo ni vyema ukajua watu hufanya makosa, wachukulie watu kama
walivyo na usiudhuke sana na kusumbua kichwa chako kwa kufikiria sana
makosa ya watu. Panapohitajika kutoa malalamiko toa na eleza kero zako,
panapohitajika kufanya linalowezekana fanya unaloweza kwa manufaa yako
na wengine ambao wanatatizwa na tatizo hilo.
5.
Kutojikubali kuwa umeshindwa na kujiona hustahili mambo yako kwenda kombo.
-Hii
hali huwatokea watu wenye uchu kupita kiasi wa kupata kitu fulani.
Sababu moja kubwa inayowafanya watu kuwa hawana furaha na maisha yao ni
kutegemea mambo makubwa bila kukubali kuwa wanaweza kushindwa. Any expectation relies on thinking about the positivities and negativities of what you expect.
Hatutakiwi kuwa na mawazo mgando kwa kufikiri chanya wakati wote bali
tufikirie hasi wakati mwingine. Ndio maana katika malengo tuna PLAN A
ikishindikana tunafuata PLAN B, C na njia nyingine mbadala za
kutufikisha tunapopataka. Ninachomaanisha hapa Don't Expect Too Much To Become Frustrated there are other many windows of opportunities for you to win.
0 comments:
Post a Comment