Dr. Wasif Saif
Maambukizi ya bakteria yanaweza kuwa ndiyo sababu kubwa inayochochea kansa
ya kongosho, kulingana na utafiti wa hivi karibuni.
Kuongezeka kwa idadi ya tafiti zinaonyesha kuwa kansa ya kongosho ina uhusiano wa karibu na bakteria wanaozalishwa kwenye tumbo na ufizi. Kulangana na tafiti mbalimbali, kansa ya kongosho ndiyo kansa hatari kuliko zote na inakadiriwa kwa mwaka huu wa 2013 itagharimu maisha ya wamarekani 38,500 kulingana na utafiti wa Dr. Wasif Saif Mkurugezi wa Programu ya tafiti za magonjwa ya utumbo Tufts Medical Center, Boston Marekani"Ni kansa inayosababisha vifo kwa kiwango cha juu zaidi na asilimia 96 ya vifo vinatokana na kansa ya kongosho”. Alisema

Ingawa kansa ya kongosho ni hatari mno, watafiti bado hawajajua kiini hasa cha chanzo chake.
Hata hivyo, inayojulikana sababu kubwa zinazosababisha kansa ya kongosho ni pamoja na uvutaji sigara, fetma, ugojwa wa kisukari sugu aina ya pili, ulevi wa kupindukia na kongosho sugu au kuvimba kwa kongosho. "Matokeo makubwa ya utafiti huu ni uwezekano kwamba maambukizi ya bakteria yinaweza kusababisha kansa ya kongosho," alisema Saif, ambaye alikuwa si mshiriki katika utafiti.
Kwa nini kansa ya kongosho, (pancreatic Cancer) ni hatari hivyo na
kupelekea kusababisha vifo vingi zaidi? Matokeo ya tafiti zilizofanywa
yaliwekwa kwenye mitandao Julai 10, 2013 katika jarida la Carcinogenesisi na mwandishi Dominique
Michaud, profesa wa magonjwa katika Chuo cha Brown Providence, RI. Maambukizi
ya wanaohusishwa na kansa
Kulingana na utafiti, wagonjwa wawili walitokana na maambukizi yaliyosababishwa na bacteria hivyo kupelekea kupata kansa ya kongosho. Takwimu zinaonyesha kwamba watu ambao wameambukizwa pylori Helicobacter, hawa ni bakteria wanaohusishwa na kansa ya tumbo na vidonda vya tumbo, na Porphyrmomonas gingivalis, maambukizi yanayotokana na magonjwa ya fizi dhaifu meno machafu. Watu wenye magonjwa haya wanaweza kukabiliwa kwa urahisi zaidi na kansa ya kongosho.

Tafiti kadhaa zimefanyika kuweza kuelezea ni namna gani magonjwa haya
yanaweza kusababisha kansa ya kongosho. Anasema Saif.
Moja ni kwamba maambukizi husababisha kuvimba kwa sehemu kubwa ya mwili, hivyo
kupelekea kupata kansa ya kongosho.
Pili maambukizi ya bakteria husababisha mabadiliko katika mfumo wa kinga wa
mwili. Wakati mfumo wa kinga ukiwa dhaifu, mwili hauwezi kujikinga na aina hii
ya saratani.
Hatari kubwa zaidi zinazosababisha kansa ya kongosho ni pamoja na kunenepa kupita kiasi, uvutaji wa sigara, na ugonjwa wa kisukari. Hivi vinaweza kukandamiza zaidi mwitikio wa kinga, na kufungua mlango kwa magonjwa nyemelezi.
Tafiti nyingine zinaonyehsa kwamba maambukizi ya bakteria yanaweza moja kwa moja kuamsha dalili za saratani ya kongosho (pancreatic tumor), kama vile wale ambao hukuza ukuaji wa seli mpya za damu na kusababisha uvimbe ambao si lazima uwe kansa lakini unaweza kusababisha kansa kwa urahisi zaidi.
Hata hivyo, wazo kwamba baadhi ya maambukizi ya bakteria yanaweza
kusababisha baadhi ya saratani si dhana mpya, Saif alisema. Watafiti wamekuwa
wakiangalia katika uhusiano huu zaidi ya muongo mmoja uliopita, na tumeona
ushahidi wa hili katika saratani ya damu na uvimbe mgumu, alielezea.
Saratani zinazohusishwa na maambukizi ni pamoja na kansa ya ini, ambayo ni inaohusishwa na hepatitis B na virusi C; kansa ya kizazi, ambayo husababishwa kwa ukaribu na virusi vya binadamu papilloma (HPV); na kansa ya koo katika pua ambayo husababishwa na na virusi vya Epstein-Barr.
Uelewa mzuri wa namna maambukizi ya bakteria katika kansa ya kongosho inaweza kutoa fursa mpya kwa ajili ya kugundua mapema na na kufuatilia matibabu mapema. Matokeo haya yanaweza kusaidia wagonjwa wa saratani ya kongosho ambao mara nyingi wanataka kujua, "Kwa nini mimi?" Saif alisema.
Kutokana na utafiti huu, watu mbalimbali au familia, wanaweza kurekebisha
tabia zao hasa kwa uvutaji wa sigara, unjwaji pombe kupita kiasi, unene mkubwa,
na hasa usafi katika fizi za meno na usafi wa kinywa kwa ujumla ili kujiweka
mbali zaidi na uwezekano wa kupata saratani ya kongosho.
Makala hii inapatikana hapa: LiveScience.com
0 comments:
Post a Comment