Wazazi wa Kang hawakuelewa mara moja ni
kwa nini tumbo la mtoto wao wa mwaka mmoja alikuwa na kitambi ambacho si
cha kawaida na kilikuwa kinakuwa kila siku.
Tumbo la Kang lilionekana na dalili zote
za ujauzito kitu ambacho kilifany amajirani waanze kujiuliza kulokoni
hadi kumpa jina la "Monster"
Lakini baada ya madaktari kumfanyia
uchunguzi mtoto huyo ambaye ana miezi 18 tu waligundua kuwa alikuwa na
hali ambayo si ya kawaida kabisa ambayo inatokea mara moja kati kesi
500,000 za kujifungua. Hii inatokea wakati mama mjamzito akiwa amemeba
mimba ya mapacha, pacha mmoja kukuwa kiukubwa kuliko pacha mwenzake na
kummeza pacha mdogo. Kwa maana hiyo kitoto kingine (foetus) hakikui ila
kinakulia ndani ya tumbo la pacha mkubwa kama parasite.
Hali hii ilimfanya Kang anayetokea katika jimbo la Henan, ashindwe kula vyakula vigumu na apatwe na maumivu makali wakati wote.
Hata hivyo, Kang anaelezwa kuwa ni mtoto
wa majanga kwani akiwa na siku chache tu tangu kuzaliwa, wazazi wake
walimwacha shambani, kilio chake ndicho kilichopelekea mfanya kazi wa
shambani Wang Ghihua kumchukua na kuishi naye kwani yeye na mume wake
Kang Xiqung hawakuwa na mtoto hivyo wazai wa Kang wakawaruhusu kukaa
naye. Walezi walishituka kuambiwa kuwa Kang alikuwa na kitotot tumboni
ambacho kilikuwa kikikandamiza viungo vyake vya ndani kadiri mimba ile
ilivyokuwa inakuwa.Kang alihitaji upasuaji ambao ungegharimu paundi
1,000 tu lakini walezi
wake walikosa, hadi msaada kutoka Msalaba Mwekundu ulivyowasili na
kuchangisha pesa kwa ajli ya kumfanyia Kang upasuaji. Upasuaji ulichukua
saa 10 na katoto kale kengine kalitolewa tumboni na sasa Kang
anaendelea kupata nafuu ya ile opereshen na atarudi kwenye maisha yake
ya kawaida. Hata hivyo upasuaji huu haukuathiri mfumo wake wa uzazi
hivyo akifikia utu uzima ataweza tena kupata watoto kama kawaida.
0 comments:
Post a Comment