Thursday, 11 July 2013

MPIGAPICHA WA MISRI AREKODI PICHA ZAKE ZA KIFO...

KUSHOTO: Ahmed Samir Assem enzi za uhai wake. KULIA: Picha iliyopigwa na Assem ikimuonesha askari akimwelekezea bunduki muda mfupi kabla ya kufyatua risasi.
Picha za kushitusha zimenasa tukio ambapo mpigapicha wa Misri alirekodi kifo chake mwenyewe kwa kutumia kamera yake.

Picha hizo zinaonesha askari wa Misri akidhamiria na kumfyatulia risasi Ahmed Samir Assem, kabla ya giza kuvamia filamu hiyo.
Mwandishi huyo mwenye miaka 26 alipigwa risasi na kufa Jumatatu iliyopit wakati akipiga picha nje ya jengo la Jeshi mjini Cairo, ambako baadhi wanaamini Rais aliyepinduliwa Mohammed Morsi amekuwa akishikiliwa.
Alikuwa ni mmoja kati ya takribani watu 51 waliouawa pale vikosi vya ulinzi vilipomimina risasi kwenye umati mkubwa wa watu ambao ulipiga kambi nje ya jengo hilo.
Assem, mpigapicha wa kujitegemea alikuwa akifanya kazi kwenye gazeti la Al-Horia Wa Al-Adala la nchini Misri.
"MAjira ya Saa 12 alfajiri, mtu mmoja alikuja kwenye kituo cha habari akiwa na kamera iliyotapakaa damu na kutueleza kwamba mwenzetu mmoja amejeruhiwa," alisema Ahmed Abu Zeid, mhariri wa utamaduni wa gazeti la Assem alieleza.
"Ndani ya saa moja baadaye, nilipokea habari kwamba Ahmed alikuwa amepigwa risasi na askari aliyekuwa mstari wa mbele wakati akipiga picha au kurekodi video juu ya majengo kwenye eneo la tukio.
"Kamera ya Ahmed ilikuwa pekee ambayo ilirekodi tukio zima kutoka mwanzo.
"Alikuwa ameanza kurekodi tangu mwanzo wa sala hivyo alinasa mwanzo kabisa na katika video, unaweza kuona mamia ya waathirika. Kamera ya Ahmed itabakia kama kipande cha ushahidi katika uhalifu uliofanyika."
Jeshi hilo limedai lilimimina risasi sababu 'kundi moja la kigaidi' lilishambulia katika jaribio la kulipua jengo hilo.
Lakini wafuasi wa Morsi walisema ufyatuaji huo wa risasi ulikuwa haukuchokozwa. Katika dondoo za kusisimua za habari, wanachama wa Muslim Brotherhood walimwita Mkuu wa Jeshi, Jenerali Abdul Fattah al-Sisi kuwa 'muuaji na chinja-chinja'.
Lakini Shehe Ahmed el-Tayeb, mfuasi wa juu wa dini ya Kiislamu nchini humo, aliasa Wamisri 'kujitwisha wajibu wao kukomesha umwagaji damu' badala ya 'kuibututa nchi hiyo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe'.
Ulinzi sasa umeimarishwa kwenye maeneo muhimu kati mji mkuu huo. Huku maandamano zaidi ya kumuunga mkono Morsi yakiwa yamepangwa, vifaru na magari yaliyosheheni silaha za kivita na wanajeshi walionekana wakirandaranda kwenye mitaa ya jiji hilo juzi usiku.
Al-Shaimaa Younes, ambaye alikuwa ameketi, alisema vikosi vya kijeshi na vikosi vya polisi viliwamiminia risasi waandamanaji wakati wa sala ya asubuhi.
"Walishambulia kwa risasi za moto na kutupa mabomu ya machozi," alisema kwa njia ya simu. "Kulikuwa na kupagawa na watu wakaanza kukimbia huku na huko. Nilishuhudia watu wakianguka."
"Wanawake na watoto walikuwa miongoni mwa waandamanaji", alisema.
Msemaji wa jeshi Kanali Ahmed Mohammed Ali alisema taarifa za awali zinaashiria kwamba watu wenye bunduki wenye uhusiano na Brotherhood walijaribu kulipua jengo la jeshi muda mfupi baada ya  mapambazuko, wakifyatua risasi za motot na kutupa mabomu kutoka kwenye msikiti wa jirani na juu ya mapaa.
"Ofisa mmoja wa polisi kwenye eneo la tukio aliuawa", alisema.
Msemaji mwingine wa jeshi alisema watu watano kutoka upande wa Brotherhood waliuawa

0 comments:

Post a Comment