Friday, 19 July 2013

MTWARA WANANCHI WACHARUKA WASHAMBULIA KWA MAWE GARI LILILOKUWA LIMEBEBA MABOMBA YA KUSAFIRISHIA GESI


Habari zilizotufikia kutoka mjini Mtwara Zinasema kuwa Gari lililobeba Shehena ya Mabomba ya Kusafirishia gesi kutoka Mjini Mtwara kuelekea Dar limeshambuliwa na mawe na kupelekea dereva Wa lori hilo Kujeruhiwa Vibaya. Lori hilo lilianza kushambuliwa mara baada ya kuingia katika manispaa ya mikinda Mtwara Mjini Sababu ya kushambulia gari hilo ni katika kile kinacho dhihirisha kua wana Mtwara bado hawajakubaliana na hoja ya Serikali ya kutaka Kusafirisha Gesi hiyo kwaajili ya Manufaa ya Nchi.

Lori hilo kwa sasa lipo kituo kikubwa cha polisi Mtwara, Ikiwani wiki moja tu imepita tokeaa watu kadhaa kukamatwa na jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kile kinachodaiwa kusambaza waraka wa kuhujumu miundombinuu yote ya gesi mara tu serikali itakapo anza utekelezaji wake wa ujenzi wa bomba hilo kupeleka Dar


0 comments:

Post a Comment